Habari Mpya

Tuesday 10 February 2015


Kutokana na ukweli kwamba viini vya vijidudu vinavyosababisha maradhi huwa havionekani kwa macho ya binadamu, inatupasa kuhakikisha usafi katika kila idara ya malezi ya mtoto. Muongozo ufuatao utamlinda mtoto walau nyumbani:

1. Nawa mikono na mfundishe mtoto utamaduni huu.

Nawa kwa kusugua mikono yote kwa maji safi na sabuni, sabuni ikikosekana tumia majivu. Mikono ni chombo kikuu cha kubeba vijidudu ambavyo huweza kusababisha magonjwa na kuvisafirisha kwenye chakula au maji atakayopewa mtoto au moja kwa moja kinywani kwa mtoto mwenyewe.


Nawa mikono:

- Unapotoka chooni

- Baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia

- Baada ya kufanya shughuli za usafi

- Kabla ya kuandaa chakula

- Kabla na baada ya kula au kumlisha mtoto

2. Tumia maji safi na salama
Maji hutumika kwa kiasi kikubwa katika shughuli mbalimbali za ustawi wa maisha ya binadamu, ni kati ya vitu muhimu sana maishani. Kuna vyanzo vingi vya maji kama mabomba, visima, mabwawa, mito n.k. na kuna jinsi mbalimbali za kuhifadhi maji kama matanki, ndoo, mitungi n.k.

Zingatia haya bila kujali chanzo cha maji:

- Chemsha maji ya kunywa siku zote na hifadhi kwenye chombo safi chenye mfuniko

- Hifadhi maji ya kunywa kwenye chombo chenye mfereji, la tumia kikombe kisafi chenye mshikio ukiwa na mikono misafi kuchota maji kutoka kwenye chombo hiki.

- Funika hifadhi zote za maji, kama visima na matanki

- Vyombo vinavyotumika kuchota maji kisimani au kwenye tanki lisilokua na mrefeji kama ndoo na kamba visafishwe mara kwa mara na kuwekwa mahali safi, kamwe visiwekwe chini

- Usitumie dawa za kuua wadudu au kemikali karibu na hifadhi au vyanzo vya maji

- Mifugo au wanyama wasikaribie hifadhi au vyanzo vya maji

3. Chakula kiive vizuri na kihifadhiwe vyema

Chakula kibichi ni makazi ya vijidudu vingi vya magonjwa, hasa vyakula vya jamii ya nyama. Vijidudu hivi hustawi na kushamiri katika joto la kawaida. Kwa kupika chakula na kukiivisha ipasavyo huua viini hivi.


Zingatia:


- Chakula kiliwe mara baada ya kupikwa

- Funika chakula kitakacholiwa baadae

- Hifadhi chakula kitakacholiwa baadae katika hali ya joto (oven) au baridi (jokofu)

- Pasha moto chakula kilichohifadhiwa kabla ya kuliwa

- Vyakula ambavyo huliwa bila kupikwa visafishwe vizuri kwa maji safi na salama




4. Ondoa takataka zote nyumbani


Takataka na mlundiko wa takataka ni mazalia mazuri ya viumbe na vijidudu vinavyosababisha magonjwa. Wadudu kama nzi, mbu, mende na panya hushamiri katika milundiko hii.





Zingatia:


- Usilale na takataka ndani, kama una sehemu maalumu ya kutupa taka ndani ya nyumba hakikisha kabla ya kulala zimetolewa na kuwekwa sehemu maalumu ya taka nje

- Usihifadhi vitu usivyokua na matumizi navyo ndani ya nyumba, kama makaratasi, maboxi, nguo n.k

- Sehemu ya nje unayotupa taka hakikisha zinaondolewa mara kwa mara ikiwa kuna huduma ya kuzoa taka, kama huduma hii haipo chimba shimo ambalo utaweza kuchoma taka hizo na kulifukia itakapobidi

- Fukia madimbwi yote, ondoa vifuu na kitu chochote kinachoweza kuruhusu maji kutuama, maji yaliyotuama ni mazalia mazuri ya mbu

5. Safisha nyumba yako
Sakafu za nyumba zetu pia hubeba viini vya vijidudu. Hii ni muhimu sana hasa kama mwanao anatambaa. Watoto hupenda sana kuweka mikono mdomoni.


Zingatia:

- Fagia na kupiga deki kila siku asubuhi kuondoa vumbi na uchafu utakaokua umejikusanya siku iliyopita

- Safisha kila inapoidi, kuna kitu kimemwagika, chombo kimevunjika n.k.

- Tumia dawa ya kuua vijidudu kwenye maji ya kupigia deki, hakikisha dekio linasafishwa na kuanikwa na tumia maji safi

- Kua na utamaduni wa kuacha viatu nje, vihifadhiwe sehemu maalumu ndani baada ya kua vimesafishwa. Viatu hubeba vijidudu vingi kutokana na sehemu ulizopita


6. Kinyesi….uuuwiii Kinyesi na choo

Kama kuna mashindano ya kubeba vijidudu, kinyesi kitaongoza siku zote, sio cha mtoto, cha mtu mzima wala cha mnyama. Usiruhusu kabisa kinyesi kuwepo mahali pa wazi.

Zingatia:

- Safisha choo kila siku na kila inapobidi

- Tumia dawa za kuua vijidudu katika kusafisha choo

- Tumia choo vizuri

- Vuta maji kila baada ya matumizi

- Kama ni choo cha shimo, hakikisha kipo umbali unaostahili na kiwe na mfuniko

- Kama mtoto anatumia diaper, hakikisha zinatupwa inavyostahili

- Watoto wasicheze karibu na choo

7. Usafi wa mwili
Piga mswaki, nawa uso, oga na umuogeshe mtoto walau mara mbili kwa siku, muhimize dada wa nyumbani kufanya vivyo hivyo. Soma zaidi jinsi ya kumuogesha mtoto, matunzo ya kucha, masikio, nywele, kitovu, sehemu za siri

8. Usafi wa vyombo
Vyombo vya mtoto, hasa mchanga, huhitaji umakini wa ziada.
- Visafishwe mara baada ya matumizi

- Viachwe vikauke na kisha kuhifadhiwa mahali mahususi kwa vyombo vya mtoto
- Visichanganywe na vyombo vingine vya nyumbani. Visilale vichafu

9. Usafi wa mavazi

10. Usafi wa malazi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top