Habari Mpya

Tuesday 10 February 2015

MAZOEZI 5 MEPESI AMBAYO YANAWEZA KUBADILI MUONEKANO WA MWILI WAKO KWA HARAKA

Mazoezi ni jambo muhimu sana kwa maisha ya wanaadamu wote katika kulinda afya za miili yao, watu wengi wamekuwa wakihangaika kufanya mazoezi kwa kuondokana na matatizo tofauti tofauti, wengine huenda wameshauriwa na Daktari kutokana na aina ya ugonjwa unaowasumbua na wengine hutaka kupunguza miili yao ili iwe katika muonekano mzuri na wengine wanataka kuilinda miili yao isije kunenepeana kiholela pia wengine hufanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea katika maisha yao.
Pengine umejiuliza sana ni jinsi gani utafanya mazoezi kutokana na muda finyu ulionao au mambo mbalimbali yanayopelekea usipate muda mwingi wa kufanya mazoezi. Katika makala hii nakuletea aina 5 za mazoezi ambazo zinaweza kukusaidia katika kuuweka sawa mwili wako na kuepukana na maradhi mbalimbali.
 1. KURUKA KAMBA
Pengine unaweza kuona ni zoezi rahisi, lakini ni miongoni mwa mazoezi ambayo yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mafuta mwilini na kuunguza calories nyingi kwa kila dakika utakayokuwa unaruka kamba. Zoezi hili halihitaji uende Gym unaweza kuruka hata na watoto wako nyumbani mmoja kashika huku na mwingine kule wewe unaingia kati unaruka, pia unaweza kuruka peke yako.


2. KUPIGA PUSHAPU
Kwa hali iliyozoeleka watu wengi wamekua wakikwepa kupiga pushapu kutokana na ugumu mdogo unaoambatana na zoezi hili.lakini hili ni miongoni mwa zoezi linaloweza kukuletea mabadiliko ya haraka zaidi katika mwili wako. zoezi la pushapu ni zuri sana kwa kukuepushia maradhi ya moyo. huhitaji kutumia nguvu sana kama unataka kupanda ulingoni ukapigane au utoke misuli, ''Hapana'' piga pushapu chache kila asubuhi na jioni kwa kadri ya uwezo wako hata kama ni 5 kwa asubuhi na 5 kwa jioni.


3. KUOGELEA
Hii ni habari njema kwa wapenzi wa kuogele, ingawa kwa watanzania tulio wengi tunachukulia kuogelea kama ni starehe tu na ni kitendo kinachopendwa na watu wachache lakini ni miongoni mwa mazoezi yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu. Kuogelea kuna shusha blood pressure, kuimarisha moyo na kuimarisha mfumo wa upumuaji. pia ni sehemu ya kufurahi na familia yako ingawa kuogelea si zoezi rahisi kama kuruka kamba na pushapu.

4. KUKIMBIA
Kuna manufaa mengi sana yanayopatikana kutokana na kukimbia, kwanza hukuondolea misongo ya mawazo, inaimarisha afya ya moyo pia inaunguza mafuta (calories) kwa kiasi kikubwa mwilini, kwa wale wenye miili minene kukimbia ni moja ya mazoezi yanayo punguza mwili kwa haraka zaidi na kutengeneza stamina kwa wanamichezo na hata wale wasiokuwa wanamichezo.


5. KUENDESHA BAISKELI
Wengi wa watanzania hudhani kuendesha Baiskeli ni umasikini, kuingia kwa bodaboda nchini kumepunguza kwa kiasi kikubwa waendesha baiskeli nchini, watu wenye vipato kidogo hujisahau na kuishia kuendesha magari tu au pikipiki na watu wa aina hii wana asilimia kubwa kuugua maradhi ya kisukari na presha, Baiskeli itakufanya utumie nguvu nyingi ambazo zita kuwa ni zoezi tosha katika kuupa mwili afya njema na kuepukana na matatizo ya sukari na presha.

MWISHO
ikumbukwe kuwa pamoja na kufanya mazoezi pia unashauriwa kupangilia vizuri mlo wako na si kufukia tu itakuwa unatia maji kwenye pakacha, hivyo basi ni lazima uzingatie mlo sahihi kwa ajili ya afya yako.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: MAZOEZI 5 MEPESI AMBAYO YANAWEZA KUBADILI MUONEKANO WA MWILI WAKO KWA HARAKA Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top