Habari Mpya

Tuesday 10 February 2015

JIKINGE NA KISONONO




Kabla ya kueleza tiba ya ugonjwa wa kisonono ni muhimu kufahamu kuwa, wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huu kwa asilimia 60 hadi 80, huku wanaume wakiwa katika hatari ya kupata ugonjwa huo kwa asilimia 20. Hii ni katika hali ambayo, kama tulivyoashiria huko nyuma dalili za ugonjwa huo huwa hazijitokezi kwa uwazi kwa wanawake ikilinganishwa na wanaume na pia ugonjwa huu una madhara zaidi kwa wanawake kwani hata huweza kuwaletea madhara watoto wao wachanga pale wanapojifungua. Hayo yote yanaonyesha umuhimu wa kutibiwa ugonjwa huo mapema hasa kwa wanawake.



Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaowapata watu wengi na Shirika la Afya Duniani WHO linakadiria kuwa watu milioni 106 duniani huambukizwa ugonjwa huo kila mwaka. Lakini je, tiba ya ugonjwa wa kisonono ni ipi? Tiba ya gono inahusishwa na tiba ya ugonjwa wa chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya mawili ya zinaa huambatana pamoja, na ili kuujua ugonjwa wa chlamydia usikose kutegea sikio kipindi chetu kijacho inshaallah.



Matibabu ya kisonono pia hutegemea umri wa mgonjwa na kama ni mwanamke, ni mjamzito au la. Kwa bahati mbaya kuhusiana na matibabu ya ugonjwa huo kumeripotiwa ongezeko la kutosikia dawa vijidudu na hivyo baadhi ya dawa zilizokuwa zikitumika huko nyuma hivi sasa zimekuwa hazina tena athari na hivyo hazitumiki tena. Kisonono ambacho sio sugu kilicho kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, hutibiwa kwa dawa za cephalosporin, ambapo mgonjwa hupewa dozi moja ya dawa hizo pamoja na dawa aina ya macrolide kwa mfano azithromycin, na za jamii ya penicillin kwa mfano doxycyclin kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa chlamydia.



Mara nyingi kwa wagonjwa walio na umri wa chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Mgonjwa hutakiwa kufuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizo kwani dawa nyingi huwa na madhara kwa wajawazito kwa mfano doxycyclin. Kwa kawaida ushauri nasaha hutolewa kwa washirika wote wawili wa ngono, na ni vizuri wote wawili watibiwe hata kama mmoja wao hatakuwa na dalili za ugonjwa huu. Mara nyingi madaktari huwapatia wale wanaosumbuliwa na kisonono dozi pia kwa ajili ya wapenzi wao hata bila ya kupimwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: JIKINGE NA KISONONO Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top