Habari Mpya

Thursday, 30 October 2014

Tanzania kushiriki Miss Grand International 2014
Warembo kutoka nchi mbali mbali walioingia fainali za Miss Grande Internationale mwaka jana. Picha na Maktaba
Kwa mara ya kwanza katika historia, mshiriki kutoka Tanzania ataliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya urembo ya kimataifa yanayofahamika kama ‘Miss Grand International 2014 (MGI) yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu Bangkok, Thailand.
Shindano hilo litajumuisha warembo kutoka zaidi ya nchi 70 duniani, litatoa fursa kwa kila mmoja kuonyesha umahiri wake katika kuwakilisha tamaduni za nchi zao hasa katika mavazi.
Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Miss Grand International Tanzania, Veronika Rovegno, alisema timu yake imejipanga kuhakikisha Tanzania inanyakua taji hilo.
“Tanzania itashiriki kwa mara ya kwanza, lakini hiyo si sababu ya kuwa wasindikizaji. Tumejipanga na tutahakikisha mshiriki wetu anakwenda Thailand kushindana na siyo kufanya majaribio,” alisema
Vero aliwataka warembo kuendelea kutuma maombi yao kwa wingi wakizingatia vigezo vyote vilivyotolewa katika tovuti ya Miss Grand International.

Hii itarahisisha katika zoezi la kufanya uchaguzi wa mwanzo kabla ya kufanyika kwa onyesho hilo nchini.
“Hivi sasa tupo kwenye mchakato wa kupokea majina na sifa za washiriki zilizoambatanishwa na picha zao, baadaye tutafanya mchujo wa mwanzo kabla la shindano lenyewe,” alisema Vero.

Mwaka jana mrembo, Janelee Chaparro kutoka Puerto Rico aliibuka mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake wapatao 70. Katika mashindano hayo Bara la Afrika liliwakilishwa na nchi za Algeria, Misri, Ethiopia, Kenya, Uganda na Zimbabwe.

mwananchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Tanzania kushiriki Miss Grand International 2014 Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top