Habari Mpya

Tuesday, 28 October 2014

AMINI USIAMINI MISS UGANDA 2014 ALIKUWA MKULIMA

Mkulima wa uyoga na mfugaji wa kuku ameteuliwa kuwa Miss Uganda 2014 kufuatia mabadiliko katika shindano hilo ambalo kwa sasa linafanya kampeni kuhusu kilimo. Leah Kalanguka, 23, aliwashinda warembo wengine 19 kwenye fainali hizo ambapo washiriki walitakiwa kukamua ng’ombe na kufanya kazi na kondoo na mbuzi.

Waandaji wa shindano hilo walishirikiana na jeshi la Uganda kulifanikisha na lengo lake ni kupromote ujasiriamali katika ufugaji kwa vijana. Katika shindano hilo, warembo waliulizwa maswali kuhusu kilimo.

Kalanguka pia amesoma computer engineering and science katika chuo kikuu cha Makerere.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: AMINI USIAMINI MISS UGANDA 2014 ALIKUWA MKULIMA Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top