(News) KINGWENDU akimbilia MSUMBUJI na mkwanja wa Director
Mchekeshaji maarufu Kingwendu anatuhumiwa
kumtapeli mtayarishaji wa filamu za kitanzania ‘Bongo Movies’ ambaye
pia ni mshindi wa tuzo za ZIFF, Bondi.
Akiongea kupitia kipindi cha Filamonata
cha 100.5 Times Fm, kinachoongozwa na Monalisa na mama yake ‘Natasha’,
Bondi amesema kuwa alimlipa pesa mchekeshaji huyo ili aweze kuigiza
kwenye filamu yake na kusaini mkataba, lakini alipotea na kuelekea
Msumbiji huku simu yake ikiwa haipatikani.
“Nilimpa fedha ya advance akachikichia
moja kwa moja kumbe ana shows zake anaenda kufanya huko Mozambique. Kwa
hiyo imefika siku ya kufanya filamu ambapo nilikuwa nashuti mimi,
Kingwendu hayupo na siku sita amezima simu haipatikani.” Amesema Bondi.
Lakini kukosekana kwa Kingwendu kulimpa
shavu mchekeshaji mwenzake Bambo, “Nikaamua nifanye option B, Option B
niliyofanya nikamtafuta Bambo nikaongea naye, nikaelewana naye vizuri na
tukafanya kazi.” Ameeleza producer Bondi.
Naye Kambarage wa kampuni ya usambazaji
wa filamu ya Steps Entertainment, amesema kwa kuwa Kingwendu amevunja
mkataba na kumuingizia Bondi gharama za ziada, kampuni ya Steps imepanga
kuongea na Kingwendu na endapo ataenda kinyume watamfungulia mashitaka
ili iwe fundisho kwa wasanii wenye tabia kama yake.
Filamonata inakuwa hewani kila Jumapili kuanzia saa 5 kamili asubuhi hadi saa 7 mchana kupitia 100.5 Times Fm.
No comments:
Post a Comment