Friday, 13 December 2013

Eti urembo wa Wolper ni nyongeza tu


JACKLINE Wolper amesema urembo wake ni nyongeza tu katika kupendezesha filamu, kwani huwa anajituma kuvaa uhusika ili aweze kufikisha ujumbe.
Wolper amefafanua kuwa wasichana wengi hufikiri kuwa urembo unatosha kumfanya awe staa hata kama hana uwezo wa kuigiza kitu ambacho si cha kweli.
“Nina uwezo ndiyo maana waandaaji wananitumia kwenye filamu nyingi, hawanichukui kwa kigezo cha urembo bali ufanyaji kazi wangu, mbona warembo wengi walijaribu fani hii lakini walishindwa,” alisema.
“Kuwa mrembo bado si kigezo cha kupendeza kwa kila unachovaa, hivyo miongoni mwa mambo yanayonifanya niwe na mafanikio na niigize filamu nyingi zenye umakini ni kutokana na kupangilia mavazi kulingana na shepu yangu na si kukurupuka kuvaa kila kinachoingia mjini,” alisema Wolper.

No comments:

Post a Comment