Wednesday, 14 November 2018
Mambo 5 usiyoyajua kuhusu matumizi ya mafuta ya nazi.
Miongoni mwa faida tano za kutumia mafuta ya nazi asilia ni:
Kulainisha ngozi:
Kuondoa magaga kwenye nyayo za miguu
kuzuia mipasuko ya nyayo za miguu
kukauka kwa ngozi ya mikononi
hivyo mafuta yanazi yanasaidia kwa kiasi kikubwa sana kulainisha ngozi na kuipa afya nzuri.
Kuondoa ngozi iliyoharibika/Dead skin:
Mafuta ya nazi husaidia kuondoa ngozi iliyoharibika katika mwili wako, ki hivii
chukua mafuta ya nazi, sukari na chumvi changanya upate mchanganyiko mmoja
kisha paka mwili mzima.
fanya massage kwa mchanganyiko huo kaa nayo kwa mda kisha kaoge vizuri na sabuni.
utaona tu mabadiliko katika ngozi yako baada ya zoezi hili.
fanya mara 3 kwa wiki au utakavyoamua wewe.
Kuondoa Make Up:
Mafuta ya nazi yanaweza pia kutumika kuondoa makeup usoni baada ya kutoka kwenye sherehe ukiwa na makeup unashauriwa kuitoa kabla ya kuingia kulala ili kuendelea na ngozi nzuri yenye afya.
Mafuta ya nazi yanatumika hivi
chukua pamba safi chovya kwenye mafuta ya nazi.
kisha anza kufuta uso wako taratibu kwa kutumia pamba iliyo na mafuta ya nazi.
baada ya kufuta chukua cleanser uliyoandaa au nawa uso wako vizuri na sabuni.
ukifanya haya utasaidia kutunza uso wako na kuwa na afya nzuri.
Kukuza nywele:
Mafuta ya nazi, yanatumika katika kurutubisha nywele na kufanya ziwe na nuru na kujaza,
kupaka kwenye ngozi
kupaka sehemu ya nywele ambazo hafifu au zilizo katika.
Kusaidia katika kunyoa/Shave oil:
Wengi wetu tumezoea kutumia Shave cream wakati wa kunyoa nywele katika maeneo maeneo lakini mafuta ya nazi pia yanaweza tumika hapa badala ya shave cream, yenyewe yanasaidia kutibu vipele vinavyojitokeza baada ya kunyoa.
haya mafuta wengi wanatumia katika kunyoa vinyweleo, inakuacha ukiwa soft na inasaidia kwa kiasi kikubwa kukufanya ngozi yako iwe salama tofauti na kutumia kiwembe au kitu kingine.
No comments:
Post a Comment