Juisi ya Tende ni miongoni mwa juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la nguvu za kiume.
MAHITAJI :
- Tende kilo moja
- Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
- Sukari kiasi upendacho.
NAMNA YA KUTENGENEZA :
- Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake.
- Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.
- Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda hadi zitakapolainika sawasawa.
- Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.
- Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
- Juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.
No comments:
Post a Comment