Tuesday, 1 December 2015

MZAZI ANACHANGIA 25% ILI KUONGEZA UFAULU KWA WATOTO MASHULENI- ENG DOROTH MTENGA



Wazazi na Walimu wametakiwa kushiriana kwa karibu ili kwa kuweza kuinua taaluma ya watoto wawapo mashuleni na hivyo kuwajengea msingi ulio bora katika maisha yao ya kila siku. 


Akizungumza wakati wa kutoa pongezi kwa Taasisi ya kielimu chini ya Shirika la Montfon Brothers katika siku ya wazazi na mahafali ya watoto shule ya awali mwaka 2015 Mgeni Rasmi Meneja wa Tanroad Mkoa wa Morogoro Injinia Doroth Mtenga amesema wazazi ni nguzo ya kwanza kwa watoto na ili wafanikiwa ni lazima wanapowapeleka shuleni wahakikishe wanashirikiana na walimu wa watoto hao kikamilifu. 

Aidha Injinia Mtenga ameipongeza shule hiyo kwa kuwa mfano bora kwa upande wa Taaluma na kuwafanya wazazi wengi kupenda kupata nafasi ya watoto wao kujiunga na shule hiyo.

Akizungumzia taaluma mwalimu wa taaluma wa Shule ya Msingi Montfon Mwl .Msuya Aston amebainisha kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vema kila wakati kwa kuwa walimu wamekuwa mstari wa mbele katika ufundishaji ulio bora unaofanya mtoto anapokuja shule hiyo anaonesha mabadiliko muda mfupi na hiyo ni sababu ya uangalizi bora wa walimu hao kwa watoto.

Aidha Mwl. Aston amebainisha kuwa, mitihani ya darasa la nne kwa awamu mbili matokeo yalikuwa mazuri ambapo watoto waliopata alama A ni 43%, B 50% na C ni 7% hivyo kwa matokeo hayo shule hiyo imeshika nafasi ya pili katika manispaa ya Morogoro. 


Vilevile kwa mitihani ya Utamilifu ambayo ilishirikisha shule 22 katika Manispaa ya Morogoro mwaka 2014 na shule hiyo imeshika nafasi ya 4.
Aidha kwa mitihani hiyo hiyo ya Utamilifu darasa la nne mwaka 2015 shule iliweza kushika nafasi ya kwanza manispaa ya Morogoro ambapo shule 87 zilishiriki na wanafunzi wote wa darasa la nne walipata alama A hiyo wamepata ufaulu wa 100%.
Lakini pia kwa watoto waliomaliza shule ya awali wameweza kufaulu kwa 98% hii inamaanisha watoto hao ni zao jema katika maisha ya baadaye endapo wazazi wataendelea kuzingatia kuwafuatilia kwa ukaribu.

Naye Mkuu wa Taasisi ya kielimu chini ya Shirika la Montfon Brothers
Jonh Paul Alexander amesema shule hiyo inatoa elimu pia kwa watoto wenye mtindio wa ubongo hivyo wanajitahidi kutengeneza mawasiliano kati ya watoto wenye matatizo ya kusikia na wale ambao hawana matatizo hayo kwa kutenga muda wa nusu saa kila siku kabla ya watoto kuingia madarasani ili kuwafundisha lugha ya alama.

Aidha shule inatoa nafasi kwa watoto kutoa hotuba kwa lugha ya kiingeleza kila siku asubuhi wanapokuwa wanajiandaa kuingia madarasani hii inasaidia kila mtoto kuweza kujiamini na kushiriki kujifunza kuongea kiingereza yeye mwenyewe wakati wote.

Pia Alexander Ameongeza kuwa mategemeo ya shule ni kuwasaidia watoto hasa wa darasa la saba mwakani kuweza kufika nafasi za juu kitaaluma.

Wakati huohuo akizungumza kwa niaba ya wazazi waliohudhuria sherehe hizo Bwana Ayubu Chuli alitoa shukrani zake kwa wazazi kufika na kuungana na uongozi wa shule na kusema hali hiyo inaonesha wote ni wamoja

 Aidha amewasifu wazazi kuwa wanafanya kazi nzuri kwa kuwaandaa watoto wao katika ujenzi wa Taifa kwani mchango wao ni Asilimia 25 hivyo wasijisahau kuona umuhimu kuwalipia chakula cha mchana kwani inamsaidia kumfanya mtoto awe makini darasani pasipo kushinda na njaa

Ameongeza kuwa watoto wanatakiwa kusaidiwa na wazazi kuibua vipaji vyao wangali wadogo hivyo kushirikiana na shule katika kuibua vibaji na kuacha kuwakataza watoto kushiriki katika michezo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment