Mwanamama mwenye umri wa miaka 35
Kim Kardashian, ambaye anajishughulisha sana na mitindo kwa sasa amebakisha
mwezi mmoja kuweza kupata mtoto wa pili amesema ameamua kuacha kwa muda mambo
ya fasheni kutokana na mabadiliko ya mwili wake
“ni ngumu kuweza kufuatilia
mitindo “ kim Kardashian alisema wakati akiongea na mwanamitindo mwenzake Guru
Andre Leon Talle katika uzinduzi wa jarida
jipya la Vorgue, Kim aliendelea kusema kuwa “marafiki zangu wananishangaa na
kusema nimeamua kuachana na mitindo na mimi nawajibu kwanini na kwa nini
unasema hivyo lakini wanasema unavaa kawaida wamekuwa wakiniona katika picha
tofauti ninazopiga kwa sasa”
Aidha si kawaida kwa Kim kwani
amekuwa akilalamikia sana kuhusu miguu yake kujaa na kushindwa kuvaa viatu
vyenye kisigino kirefu, huku akicheka alisema " imefikia wakati sasa miguu
yangu imekuwa ikijaa ingawa sio kama ilivyokuwa mwanzo lakini ndio ipo hivyo
kwakweli nipo mwishoni kwa kuwa na hali hii naamini siku itafika na nitarudi
katika hali yangu ya kawaida katika mitindo”
Hata hivyo mimba yake haimzuii
kufanya mpangilio mzuri wa chakula chake cha kila siku hivyo amekuwa
akifuatilia ulaji wake kwa kuzingatia milo yote mitatu katika ubora hasa katika
hali aliyonayo
“kila asubuhi nakula mayai meupe
na maparachichi, pia uji lakini kwa mchana napenda salad na usiku nakuala risotto
au tambi”.alisema Kardashian
Kimkardashian sio mpenzi sana na
kutoa shukrani ya chakula lakini amebainisha kutakuwa na zoezi hilo mwaka huu
nyumbani kwa mama yake Kris Jenner hapo ndipo anapoona mabadiliko na kipindi
baba yake alipowazoesha kufanya shukrani hizo kipindi cha nyuma
“kila tunapotoa shukrani huwa mapumziko na baba yangu lakini kwa sasa
tunaenda kwa ndugu tofauti mfano nyumbani kwa dada yangu hii ni mabadiliko ya
kimila” alisema Kardashian
Mwanamama huyo amebakisha mwezi
mmoja kuweza kupokea mtoto mwingine baada ya North West ambaye atamkaribisha
mdogowake toka kwa mama yake huyo, anayezaa na mwanamuziki Kanye West
No comments:
Post a Comment