Habari Mpya

Monday, 10 November 2014

Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, ajivua mwenyeweLilian ambae ndio amevishwa taji hilo kwa sasa ni wa kwanza kutoka kulia.
Tangu Sitti Mtemvu atangazwe mshindi pale Mlimani City kumekua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Watanzania yalifuatia kutokana na umri wake pamoja na taarifa nyingine ambazo yeye alizikanusha na kusema ni uzushi ikiwemo ya kuwa na mtoto.

Baada ya haya yote Novemba 8, 2014 Kamati ya Miss Tanzania imekutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo ikamtangaza ambaye atashikilia taji hilo kwamba ni mshindi namba mbili wa Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, ajivua mwenyewe Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top