Habari Mpya

Friday 17 October 2014

Ana miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters) madai ya mrembo wetu Miss TZ 2014


 Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo. Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji. 

Mshtuko! Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014,
 Sitti Abbas Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake 
kutokana na utata wa umri wake, Ijumaa limesheheni data. 


Mara baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa 
chini zilidai kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18
 na elimu ya (digrii mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua 
wengi na kuanza kuhoji uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango
 chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza 
darasa la kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
 
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi. ELIMU YA BONGO IKOJE?
Kwa mfumo wa elimu nchini ulivyo, mtoto huanza darasa la
 kwanza akiwa na kati ya miaka mitano hadi saba, jambo
 ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani hesabu zinakataa 
hata kwa mtu asiyesomea mahesabu. 
Ukiachilia mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua 
kati ya miaka miwili hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya 
elimu ya msingi (primary), miaka minne ya sekondari (ordinary level), 
miaka miwili ya kidato cha tano na sita (advanced level) na miaka
 mitatu ya shahada kwanza (bachelor degree), jumla ni miaka 16. 
 
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. Pia kuna madai kwamba 
ametumia mwaka mmoja kusomea shahada ya pili (masters) huku 
kukiwa na muda ambao kwa kawaida huwa unapotea baada ya
 kumaliza kidato cha nne kwenda cha tano na baada ya kumaliza kidato 
cha sita kwenda chuo kikuu. 
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA 
MIAKA MIWILI?
Kwa mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi
 atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo 
ambalo ni msamiati mpya kwa jamii ya Kibongo.
 
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki 
zake wa mamtoni. BABA MZAZI ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata
na tafrani inayoendelea kwenye mitandao
 ya kijamii hadi kufikia hatua ya watu kutukanana, gazeti hili 
lilimtafuta baba mzazi wa Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, 
Dar kwa leseni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Abbas 
Zuberi Mtemvu alipopatikana alifunguka:
“Umri wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile (miaka 18),
 kama mnataka kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania 
mtaoneshwa passport (hati ya kusafiria) yake…,” alisema mzazi huyo
 huku akiomba aachwe kwanza ashughulikie wananchi wa jimboni kwake. 
Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akiwa na baba yake,
 Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu. 
TUMUAMINI MZAZI?
Hata kama tukiamini maelezo ya mzazi, maana yake 
ni kwamba mrembo huyo alianza darasa la kwanza akiwa 
na miaka miwili, jambo ambalo linazidi kuongeza utata katika 
sakata hilo. 
AKATAA KUHITIMU MASTERS
Alipobanwa zaidi kuhusu taarifa zinazosema kuwa mwanaye amehitimu masters, mzazi huyo alikanusha na kudai kwamba mwanaye amehitimu bachelor degree(shahada).
“Kuhusu masters mnakosea, mwanangu hana masters, ana bachelor, nilimshauri achukue masters lakini akaomba nimuache ashiriki kwanza mashindano ya u-miss ndiyo aje aendelee baadaye,” alisema mheshimiwa huyo.
 
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu wakati wa kutwaa taji
NI AIBU NYINGINE KWA LUNDENGA?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, suala la warembo
 kudanganya umri limekuwa ni sugu hivyo kuleta tafsiri ya aibu 
kwa muandaaji wa mshindano hayo, Hashim Lundenga akidaiwa kupigwa changa la macho pindi anapowapokea katika mchakato wa awali.
Pasipoti ya kusafiria ya 
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. “Hii ni aibu 
nyingine kwa Lundenga kwani haiwezekani mtu akaingia akasema 
ana miaka kumi na nane halafu awe na elimu kama hiyo, 
anashindwaje kulibaini hilo mapema?” Alihoji mdau mkubwa 
wa urembo nchini akikumbushia kisa cha Wema Isaac Sepetu,
 Miss Tanzania 2006/07 ambaye naye alidanganya umri akasema
 ana miaka 18 wakati alikuwa na kumi na saba.
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu. MSIKIE LUNDENGA
 SASA
Alipotafutwa Lundenga ili kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa
 kifupi na kukata simu:
“I can’t answer that question (Siwezi kujibu swali hilo)…siwezi.”
SITTI ANASTAHILI KUWA NA UMRI GANI?
Ukiachilia mbali muonekano, baadhi ya watu waliozungumza na 
gazeti hili walisema kuwa ukifuata utaratibu wa mfumo wa elimu 
Bongo, Sitti alipaswa angalau awe na umri wa miaka 23, hata kama 
madai ya kurushwa madarasa ni sahihi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Ana miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters) madai ya mrembo wetu Miss TZ 2014 Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top