Habari Mpya

Monday, 25 August 2014

Nguo za zamani hazina nafasi kwa sasa- LINA SANGA

Msanii machachari wa kike  Linah Sanga amefunguka na kudai kuwa huwa anapoenda nyumbani kwa wazazi wake huwa anavaa nguo ndefu tena za kilokole zaidi ili asije kuwaudhi wazazi wake ambao wamemkuza katika maisha hayo.

Msanii huyo anapenda kuishi kizungu baada ya kuigia kwenye muziki, ingawa anadai kuwa hawezi kusahau maisha ya kidini aliyokuwa anaishi awali ambayo yalikuwa yanamfanya avae nguo za heshima tofauti na sasa.

Linah alidai kuwa tangu alipoachana na wazazi wake maisha yake yamekuwa tofauti kwani muziki kwa upande fulani umebandilisha maisha yake, kuanzia kwenye mavazi tabia na hata lifestyle.


“Napozungumza tabia haimanishi nimekuwa muhuni hapana, bali awali nilikuwa sijuani na watu maarufu lakini sasa nimekuwa nao karibu na kuna baadhi ya vitabia nimekuwa navyo lakini si kwa ubaya,” alidai.

Msanii huyo aliongeza kuwa wazazi wake wamekuwa wakimsihi sana kuvaa nguo zile zile za zamani lakini haoni kama zina nafasi kwa sasa kutokana na career aliyoichagua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Nguo za zamani hazina nafasi kwa sasa- LINA SANGA Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top