Habari Mpya

Saturday, 9 August 2014

Ndugu wa Beyonce azungumzia ugomvi wake na Jay Z

Jay Z akiwa na shemeji yake Solange Knowles, wawili hao walikuwa na ugomvi miezi miwili iliyopita ambao wameshaupatia suluhisho.
Jay Z akiwa na shemeji yake Solange Knowles, wawili hao walikuwa na ugomvi miezi miwili iliyopita ambao wameshaupatia suluhisho.

Shemeji wa Jay Z, Solange Knowles, ameamua kufunguka juu ya ugomvi wake na Jay Z, ambapo wawili hao walionekana kwenye vipande vya video zilizovuja, wakiwa wanapigana ndani ya lifti huku Beyonce akiwashuhudia pasipo kufanya uamuzi wowote wakuwatafutia suluhisho.
Baada ya tukio hilo kutokea Solange hakuweza kulizungumzia kwenye vyombo vya habari kwani alihisi ni mambo ya kifamilia ambayo siyo lazima kuyaweka hadharani.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Jarida maarufu la nchini Marekani la Lucky Magazine, alisema analichukulia tukio hilo alilolifanya na shemeji yake kama hadithi za zamani na kwamba kwa sasa wameshapatana na wanashirikiana katika kila jambo kama watoto wa familia moja.
Aliendelea kusema kuwa kitu muhimu kwake kwa sasa ni kuwa, familia yake inaishi kwa amani na kila mtu anafurahia uwepo wa mwenzie katika maisha.
Video hiyo ilivuja wiki moja baada ya tukio hilo kutokea Mei 5, ilimuonesha Solange akimrushia mateke pamoja na ngumi shemeji yake.

Jay Z pamoja na Solange wote walikubali kuwajibika kuhusiana na tukio hilo na walisikika wakiomba radhi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Beyonce and Jay Z's Hottest Moments on Stage
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Ndugu wa Beyonce azungumzia ugomvi wake na Jay Z Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top