Habari Mpya

Sunday, 15 June 2014

KUONDOA WEUSI KWENYE MIDOMO...NA HATA KWAPANI..

Mara nyingi makwapa jubadilika rangi na kuwa meusi na inabidi mara kwa mara tuondoe nywele za kwapani.Ila tatizo linakuja makwapa kuwa meusi,ni unyoaji mbaya,vitu tunavyopaka kama deodorant au nini msaada tafadhali na huo weusi unatolewaje.
Midomo ni kiungo katika mwili ambacho pia kina hitaji matunzo,kuna mwenzetu midomo yake imebadilika rangi kutokana na uvutaji wa sigara kwa muda sasa.Anataka midomo irejee katika hali yake ya kawaida anaomba msaada wa ushauri afanyeje kuondoa weusi huo na mbaya zaidi kuna saa midomo ina mkauka kwelikweli,mie nimempa ushauri wangu lakini wa kwako pia unahitajika.

 NJIA ZA KUWEZA KUKUSAIDIA KUONDOKANA NA TATIZO HILI

Jinsi ya kuondoa rangi ya nyeusi ya midomo na makwapa inatakiwa kwanza uwe tayari kwa kubadilika na kufuatilia njia hizi, leo ntakupa njia chache za kukusaidia kuondoa weusi wa makwapa na midomo.

Ili ufanikiwe kuweza kuondoa weusi wa makwapa kwanza unatakiwa kuhepuka unyoaji wa mara kwa mara, vilevile uangalie aina ya deodorant unayotumia, kuna baadhi deodorant zina kemikali ambazo ukiitumia husababisha weusi katika makwapa lakini kama tayari umekwishajikuta una tatizo hilo jitahidi chukua limao kata kipande sugua kwapani na uache majimaji yake yakauke kabla ya kuvaa nguo yako.
ukishakauka kaa nayo kwa muda wa dk 20 na unawe baada ya hapo unaweza ukavaa nguo yako na kuendelea na shuguli zako za kawaida, fanya zoezi hili mpaka utakapoona mabadiliko.

Kwaupande wa watumiaji wa sigara au pombe kali lazima tatizo hili linawakuta maranyingi unachotakiwa kufanya acha kuvuta sigara au kutumia pombe kali maana huunguza layer ya juu ya ngozi ya mdomo, hakikisha unafanya hivyo alafu nunua lip bum kwa wanaume upake ili kulainisha midomo yako na kwa wanawake unawezakutumia hata lipshine kulainisha ngozi ya midomo lakini pia zingatia kupitisha mswaki kwenye lips zako kila unaposwaki asubuhi na hata wakati wa kulala.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: KUONDOA WEUSI KWENYE MIDOMO...NA HATA KWAPANI.. Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top