Habari Mpya

Friday 22 November 2013

Utunzaji wa Mikono na Miguu


beautiful_feet

Miguu kama sehemu nyingine za mwili isipoangaliwa vizuri huweza leta madhara kiafya. Ni vizuri miguu ikatunzwa vizuri kuanzia viatu vinavyovaliwa hadi jinsi ya kuisafisha. Kuna aina mbalimbali za viatu mfano viatu vya kufunika vifupi, viatu virefu vya wazi, viatu vifupi vya wazi na viati virefu vya kufunika. Viatu vyote hivi huwa vinakuwa na muundo tofauti kadiri mvaaji anavyopendelea.

Ni vizuri kuepuka kuvaa viatu virefu sana mara kwa mara na hasa kama unatembea navyo kwa muda mrefu maana husababisha matatizo kwenye misuli ya miguu kama vikivaliwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia ni vyema kutovaa viatu vya kufunika na vyenye joto sana kwa muda mrefu hasa sehemu zenye joto kali maana huweza leta matatizo kwenye miguu. Vile vile si vyema kuvaa viatu vya wazi nje kama sehemu inabaridi kali na barafu.

Ili miguu yako iweze kuwa na uzuri wa asili siku zote basi ni vizuri angalau mara moja kwa wiki uwe na siku maalumu ya kusafisha miguu yako (sio kwamba siku nyingine husafishi, la hasha hapa naongelea usafi maalum). Andaa maji ya uvuguvugu na uweke nyenye beseni pamoja na sabuni ya maji ambayo ina dawa (medicated).  Kisha kata kucha zako vizuri na kama utapendelea basi uisugue miguu yako kwa kutumia mafuta maalumu ya kusugulia kuanzia kwenye magoti hadi vidoleni (scrub).Kisha loweka kwenye maji kwa muda wa dakika tano.

Baada ya hapo nawa vizuri na kusugua unyayo kwa kifaa maalumu au jiwe laini kisha suuza miguu yako na maji safi. Baada ya hapo kausha vizuri na upake mafuta mazuri kwa ajili ya kulinda ngozi ya miguu. Hakikisha uchafu wote umetoka na hasa kwenye kucha na vidole.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Utunzaji wa Mikono na Miguu Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top