Habari Mpya

Wednesday, 14 November 2018

Fahamu jinsi ya kutengeneza Juice ya Tende na faida zake

Juisi ina faida nyingi katika mwili wa binadamu, zipo juisi za aina mbalimbali ambazo zinatokana na mimea na mizizi aliyoumba Mwenyezi Mungu.
Juisi ya Tende ni miongoni mwa juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la nguvu za kiume.

MAHITAJI :
  • Tende kilo moja
  • Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
  • Sukari kiasi upendacho.
KUMBUKA : Tende zina asili ya sukari hivyo hakikisha unaweka kiasi kidogo.
NAMNA YA KUTENGENEZA :
  • Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake.
  • Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.
  • Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda hadi zitakapolainika sawasawa.
  • Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.
  • Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
  • Juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.
Next
This is the most recent post.
Older Post
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Fahamu jinsi ya kutengeneza Juice ya Tende na faida zake Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top