Baraza
la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa iliyotolewa na waandaaji
wa shindano la Miss Tanzania ya LINO Agency, kwamba Baraza hilo ni moja
ya chanzo cha kukwamisha shindano hilo kufanyika.
PICHA NA MTANDAO
Kweye
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, BASATA imesema ilitoa kibali
cha muda kwa kampuni hiyo kuweza kushughulikia matatizo yake, pamoja na
kuratibu safari ya Miss Tanzania 2017 aliyeshiriki mashindano ya Miss
World mwaka huu.
Taarifa
hiyo imeendelea kwa kutoa wito kwa makampuni yanayoandaa mashindano ya
sanaa kuongeza weledi, na kuzingatia sheria, ili kuepuka matatizo kama
hayo.
0 comments:
Post a Comment