Kasi ya
Mawaziri wa Rais John Pombe Magufuli kufanya ziara za kushtukiza na kutoa
maagizo kwa watendaji imeanza kufumua uozo baada ya jana kubainika kuwa
watumishi 219 kati ya 704 wa serikali wameajiriwa kwa vyeti vya kughushi.
Sakata
hilo liliibuliwa baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kutembelea
Idara,vitengo vya Usimamizi wa Rasilimaliwatu (Utumishi) na
kuagiza hatua kali zichukuliwe kwa wote waliobanika kutumia vyeti visivyo vyao
kupata ajira serikalini.
“Watumishi
wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi
wa Umma (Payroll), kwamba wametumia vyeti visivyo halali wachukuliwe hatua
stahiki,” amesema
Kairuki.
Amemtaka
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa RasilimaliwatuUtumishi, Emmanuel Mlay
kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya
kughushi.
“Muwasilishe
vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki
muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali
kwao,”
alisisitiza.
Naye,
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa RasilimaliwatuUtumishi, Leonard
Mchau, alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imehakiki
watumishi 704 na kati ya hao, watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na
Baraza la Mitihani, waligundulika waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.
Hata
hivyo, Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao waliobainika kughushi vyeti
ili kujipatia ajira serikalini, wamekimbia vituo vyao vya kazi. Mchau aliwaasa
wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti, ili kujipatia ajira Serikalini.
“Ni kosa
la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi, sasa endapo utagundulika
umeghushi vyeti, utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alifafanua Mchau.
Kwa
sasa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na uhakiki wa
vyeti kwa watumishi wote wa umma nchini mpaka kila mmoja atakapohakikiwa.
No comments:
Post a Comment