Wazazi
na Walimu wametakiwa kushiriana kwa karibu ili kwa kuweza kuinua taaluma ya
watoto wawapo mashuleni na hivyo kuwajengea msingi ulio bora katika maisha yao
ya kila siku.
Akizungumza
wakati wa kutoa pongezi kwa Taasisi ya kielimu chini ya Shirika la Montfon Brothers
katika siku ya wazazi na mahafali ya watoto shule ya awali mwaka 2015 Mgeni
Rasmi Meneja wa Tanroad Mkoa wa Morogoro Injinia Doroth Mtenga amesema wazazi ni nguzo ya kwanza kwa watoto na ili wafanikiwa
ni lazima wanapowapeleka shuleni wahakikishe wanashirikiana na walimu wa watoto
hao kikamilifu.
Aidha
Injinia Mtenga ameipongeza shule hiyo kwa kuwa mfano bora kwa upande wa Taaluma
na kuwafanya wazazi wengi kupenda kupata nafasi ya watoto wao kujiunga na shule
hiyo.
Akizungumzia
taaluma mwalimu wa taaluma wa Shule ya Msingi Montfon Mwl .Msuya Aston amebainisha
kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vema kila wakati kwa kuwa walimu wamekuwa
mstari wa mbele katika ufundishaji ulio bora unaofanya mtoto anapokuja shule
hiyo anaonesha mabadiliko muda mfupi na hiyo ni sababu ya uangalizi bora wa
walimu hao kwa watoto.
Aidha
Mwl. Aston amebainisha kuwa, mitihani ya darasa la nne kwa awamu mbili matokeo
yalikuwa mazuri ambapo watoto waliopata alama A ni 43%, B 50% na C ni 7% hivyo
kwa matokeo hayo shule hiyo imeshika nafasi ya pili katika manispaa ya
Morogoro.
Vilevile
kwa mitihani ya Utamilifu ambayo ilishirikisha shule 22 katika Manispaa ya
Morogoro mwaka 2014 na shule hiyo imeshika nafasi ya 4.
Aidha
kwa mitihani hiyo hiyo ya Utamilifu darasa la nne mwaka 2015 shule iliweza
kushika nafasi ya kwanza manispaa ya Morogoro ambapo shule 87 zilishiriki na
wanafunzi wote wa darasa la nne walipata alama A hiyo wamepata ufaulu wa 100%.
Lakini
pia kwa watoto waliomaliza shule ya awali wameweza kufaulu kwa 98% hii
inamaanisha watoto hao ni zao jema katika maisha ya baadaye endapo wazazi
wataendelea kuzingatia kuwafuatilia kwa ukaribu.
Naye
Mkuu wa Taasisi ya kielimu chini ya Shirika la Montfon Brothers
Jonh Paul Alexander amesema shule hiyo inatoa elimu pia kwa watoto wenye mtindio wa ubongo hivyo wanajitahidi kutengeneza mawasiliano kati ya watoto wenye matatizo ya kusikia na wale ambao hawana matatizo hayo kwa kutenga muda wa nusu saa kila siku kabla ya watoto kuingia madarasani ili kuwafundisha lugha ya alama.
Jonh Paul Alexander amesema shule hiyo inatoa elimu pia kwa watoto wenye mtindio wa ubongo hivyo wanajitahidi kutengeneza mawasiliano kati ya watoto wenye matatizo ya kusikia na wale ambao hawana matatizo hayo kwa kutenga muda wa nusu saa kila siku kabla ya watoto kuingia madarasani ili kuwafundisha lugha ya alama.
Aidha
shule inatoa nafasi kwa watoto kutoa hotuba kwa lugha ya kiingeleza kila siku
asubuhi wanapokuwa wanajiandaa kuingia madarasani hii inasaidia kila mtoto
kuweza kujiamini na kushiriki kujifunza kuongea kiingereza yeye mwenyewe wakati
wote.
Pia
Alexander Ameongeza kuwa mategemeo ya shule ni kuwasaidia watoto hasa wa darasa
la saba mwakani kuweza kufika nafasi za juu kitaaluma.
Wakati
huohuo akizungumza kwa niaba ya wazazi waliohudhuria sherehe hizo Bwana Ayubu
Chuli alitoa shukrani zake kwa wazazi kufika na kuungana na uongozi wa shule na
kusema hali hiyo inaonesha wote ni wamoja
Aidha amewasifu wazazi kuwa wanafanya kazi
nzuri kwa kuwaandaa watoto wao katika ujenzi wa Taifa kwani mchango wao ni Asilimia
25 hivyo wasijisahau kuona umuhimu kuwalipia chakula cha mchana kwani inamsaidia
kumfanya mtoto awe makini darasani pasipo kushinda na njaa
Ameongeza
kuwa watoto wanatakiwa kusaidiwa na wazazi kuibua vipaji vyao wangali wadogo
hivyo kushirikiana na shule katika kuibua vibaji na kuacha kuwakataza watoto
kushiriki katika michezo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment