Habari Mpya

Monday, 4 May 2015

MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA KIZAZI/UZAZI..!!




MIMBA inayotungia nje ya mfuko wa uzazi kwa kitaalamu inafahamika kama ectopic
pregnancy. Hii mimba inayotungia nje ya mfuko wa kizazi huwa inakaa ndani ya mirija ya uzazi. Mimba kama hii huwa anaipatapa mwanamke kwa njia ya kawaida au anaweza kuipata kwa njia ya upandikizaji.

Mimba hii inaweza kutoa ndani ya mirija ya uzazi ila wataalamu wanasema kwamba zaidi ya asilimia 97 huwa inatokea kwenye mirija ya uzazi.

SABABU.
Uharibifu wa Mirija ya uzazi
Mara nyingi uharibifu wa mirija ya uzazi kwa njia yoyote ile ndio huwa inapelekea kutokea
kwa utungaji wa mimba nje ya mfuko wa uzazi ambayo hujiotesha katika mirija ya uzazi na hatima yake huleta shida na matatizo makubwa.

Kwanza ieleweke mwanamke anaweza kupata mimba hii bila sababu yoyote na si kila mwanamke ambaye anapata ectopic pregnancy aliwahi kuwa na kisababishi fulani.

Lakini wanawake wengi wanapata hizi mimba kutokana na sababu nyingi mbalimbali. Mara
nyingi mwanamke ambaye alishawahi kupata mimba ambayo imetunga nje ya mfuko wa uzazi ana hatari tena ya kupata tatizo hili.

Kujaa maji kwa mirija ya uzazi
Tatizo la kujaa maji kwa mirija ya uzazi linaweza kusababisha mimba kutunga nje ya
mfuko wa uzazi. Kama mrija mmoja wa mwanamke utakuwa na maji ukazuia yai moja kupita na mimba ikatunga pale pale hata kama mrija huo utakatwa maambukizi yatakuwa yashahamia katika mrija wa upande wa pili.

Kwa hiyo mwanamke ana hatari ya kupata tena mimba itakayotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Kutokea kwa vimbe mbalimbali katika mfuko wa kizazi Kuna viti vingi ambavyo huweza kusababisha tatizo hili ikiwemo pia kutokea kwa vimbe katika mirija ya uzazi nazo huweza kusababisha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi.

Maambukizi ya magonjwa ya ngono Tatizo jingine ambalo linaweza kusababisha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni maambukizi ya magojwa ya ngono kama gonorea na magonjwa ya zinaa.

Hivyo mwanamke ambaye ameugua magonjwa haya huko nyuma ana hatari kubwa ya kupata ectopic pregnancy kwa sababu madaktari wanasema kitendo cha kuugua magojwa ya ngono kinamsababishia wanamke kupata tatizo la PID.

Lakini si magojwa ya ngono pekee hata yale ambayo hayaambukizwi. Wako bacteria mbalimbali ambao mwanamke anaweza kuwapata kupitia njia mbalimbali nao wanaweza kufanya tatizo hili.

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi Kwa kawaida mimba ambayo inatungia nje ya uzazi muda mwingi huwa haionyeshi dalili hadi pale zinapokaribia wiki sita au nane baada ya mwanamke kuona hedhi yake ya mwisho.

Kwa ukubwa wa mimba ile inaweza kuwa tayari ikawa imeshazidi uwezo wa kuhimili uwezo wa mirija ya uzazi na hivyo kumfanya mwanamke kupata maumivu makali tumboni chini ya kitovu.

Kuona siku wakati ni mjamzito Dalili nyingine ni mwanamke kupata matone
ya damu wakati mwanamke ni mjamzito. Hii ni moja ya dalili lakini dalili nyingine ambayo ni mbaya zaidi ni pale mwanamke ambapo anakuwa na mimba ambayo imetungia nje ya mfuko wa uzazi na ikaendelea kukua hufikia wakati ikapelekea kupasuka kwa mirija ya uzazi na kusababisha mshipa mkubwa wa damu ambao ni Ateri kupasuka na hatimaye kumwaga damu nyingi tumboni.

Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu. Yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba. Na muda mwingine mwanamke hupoteza fahamu.

Matibabu
Matibabu ya mimba iliyotunga nje ya kizazi yanaweza kuwa ya aina mbili.

Aina ya kwanza ni kwa njia ya upasuaji na aina ya pili ni kwa kutumia dawa mbadala ..
WAHI MAPEMA KUMUONA DAKTARI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA KIZAZI/UZAZI..!! Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top