Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na
usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo
zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika
ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.
Mahitaji
Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil
Matayarisho
Mmarinate
samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya
hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza
kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi
katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki
wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia
kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea
kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha
zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao
kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato
wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.
0 comments:
Post a Comment