Kwa mara ya kwanza katika historia, mshiriki kutoka Tanzania
ataliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya urembo ya kimataifa
yanayofahamika kama ‘Miss Grand International 2014 (MGI) yatakayofanyika
mwishoni mwa mwaka huu Bangkok, Thailand.
Shindano
hilo litajumuisha warembo kutoka zaidi ya nchi 70 duniani, litatoa fursa
kwa kila mmoja kuonyesha umahiri wake katika kuwakilisha tamaduni za
nchi zao hasa katika mavazi.
Akizungumza na gazeti hili
Mkurugenzi wa Miss Grand International Tanzania, Veronika Rovegno,
alisema timu yake imejipanga kuhakikisha Tanzania inanyakua taji hilo.
“Tanzania
itashiriki kwa mara ya kwanza, lakini hiyo si sababu ya kuwa
wasindikizaji. Tumejipanga na tutahakikisha mshiriki wetu anakwenda
Thailand kushindana na siyo kufanya majaribio,” alisema
Vero
aliwataka warembo kuendelea kutuma maombi yao kwa wingi wakizingatia
vigezo vyote vilivyotolewa katika tovuti ya Miss Grand International.
Hii itarahisisha katika zoezi la kufanya uchaguzi wa mwanzo kabla ya kufanyika kwa onyesho hilo nchini.
“Hivi
sasa tupo kwenye mchakato wa kupokea majina na sifa za washiriki
zilizoambatanishwa na picha zao, baadaye tutafanya mchujo wa mwanzo
kabla la shindano lenyewe,” alisema Vero.
Mwaka jana mrembo, Janelee Chaparro kutoka Puerto Rico aliibuka mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake wapatao 70. Katika mashindano hayo Bara la Afrika liliwakilishwa na nchi za Algeria, Misri, Ethiopia, Kenya, Uganda na Zimbabwe.
mwananchi.
0 comments:
Post a Comment