.
Tanzania-New York based model Millen Magese, ambaye alishinda taji la Miss Tanzania na kuiwakilisa nchi katika mashindano ya Miss world nchini Afrika kusini, alizaliwa tar 22 September 1982
Leo amekuja kuhamasisha wanawake kufahamu tatizo
linalomkabili mpaka kupelekea kuwa gumu katika maisha yake ingawa anajitahidi
kulikubali, Millen anasema hakuna mwanamke asiyependa kuwa mama lakini endapo
utakumbwa na tatizo kama la kwake kuna njia nyingine ambazo zinaweza kumsaidia
mwanamke asiwe mpweke kwa kukosa mtoto, kuna njia ya kupandikiza mayai, kuna
njia ya kupandikiza mayai yako kwa mwanamke mwingine lakini pia kuna njia ya
kurithi watoto na ukajiskia kama mwanamke mwingine ambaye ni mama.
Imekuwa kawaida kwa wanawake wafikapo katika siku zao za
hedhi kuumwa tumbo na kuona ni kawaida, millen happiness magese anasema kuumwa
tumbo ni kawaida lakini usiumwe kupitiliza hilo ni tatizo, "endapo utaumwa
na kulazwa, kutapika sana, kuchoma sindano tambua unatatizo hiyo si hali ya
kawaida" imekuwa kawaida kwake kipindi chote alichokua akisoma kuugua kwa
kupitiliza na ikifika wakati katika maisha yake ya shule kufanya kitu fulani na
wenzake kugundua ataumwa kunabaki pengo kubwa na katika team hiyo kunaonekana
upungufu " ilifika wakati hata tukiwa tunasafiri kuelekea katika michezo
na nikiwa naumwa basi lazima inafika mahala gari itasimama na mie ntatolewa nje
kwa ajili ya kuchoma sindano ndipo ntajiskia vema, na hii imenipelekea nikawa
najichoma sindano mwenyewe".
Ni tatizo alilodumu nalo tangu akiwa shuleni bila kufahamu
anaugua nini lakini baada ya kukutana na Jane ambaye amekua mtu wakaribu sana
katika maisha yake hasa kipindi alipofika south afrika na kumwona anafaa kuingia
katika mambo ya modeling akamuamini na ndipo akawa mlezi wake wa karibu
marazote alipokuwa akiumwa, tangu afahamike na tatizo hilo amekwishafanya
oparation 10 na mbili kati ya hizo alifanyia Marekani.
Imefikia wakati Tanzania ianzishe Hospitali ya wanawake ili kuwalinda na
kuwajali kwani wanawake wakijaliwa ni rahisi kuwa na familia bora na zenye afya
njema, Millen akusita kutoa shukrani zake nyingi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kumpokea na kumsiliza jambo lake pia kusema ni jambo zuri ambalo kila
mtanzania anatakiwa kufahamu, mambo ya uzazi nchini yamekuwa yakifichwa fichwa
kutokana na utamaduni wetu lakini endapo matatizo yakifichwa basi tunapelekea
matatizo kukua wakati njia zipo za kuweza kuwasaidia watu kuepukana na
matatizo.Ni mmoja ya wanawake wanaojitoa kusaidia wengine kutambua na kushughulikia tatizo hili kabla ya halijawa kubwa kushindwa kutibika kama ilivyo kuwa kwake, hivyo yupo tanzania kwa ajili hiyo
Fashion Time na Tatyana Celestine blogspot inaunga mkono kwa asilimia mia kufanikisha zoezi hilo hapa Tanzania wote tujumuike pale Cocobeach siku ya jumapili kuweza kusikia nini hasa kinamsumbua Millen Magese pia kujua njia ambazo zinaweza kukusaidia kuhepuka tatizo hilo.
Ama kwa hakika kwa majina aliwaita watu maharufu kama Wema Sepetu, Diamond Platnum, Faraja Kota, Lady Jay Dee na wengine wengi ili kusaidia kufanikisha kufahamisha jamii kuhusu tatizo hili ambalo kwake ni maumivu na limemsumbua kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment