Habari Mpya

Tuesday, 4 February 2014

KWA NGOZI NYORORO YENYE KUWAKA, NISIKILIZE MIMI SASA...



KILA mtu anapenda kuwa na ngozi laini na ya kuvutia, kuna wengine wanafanikiwa kuwa na ngozi hizo lakini wengine wanashindwa kuwa na ngozi laini kama ya mtoto kutokana na kukosea baadhi ya mambo.

Makala ya leo inachambua hatua muhimu za kuhakikisha unakuwa na ngozi laini wakati wote.

Kitu cha kwanza cha kuzingatia ni kuhakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kung'ang'ania na kufanya uso usiwe na mng'ao wa asili na husaidia kuzuia chunusi.

Kitu kingine ni kuhakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inakwenda sawa na ngozi yako, kama ngozi yako ni ya mafuta hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na unyevu kiasi (sabuni hizo zinapatikana kwenye maduka ya vipodozi).

Vile vile mhusika anatakiwa kuwa na krimu mbili, yaani ile inayopaswa kupaka mchana na ya usiku. Ikumbukwe kuwa wakati wa usiku ngozi inatakiwa kupakwa krimu laini zaidi kuliko mchana.

Mhusika pia anatakiwa kusugua ngozi yake au kufanya 'scrub' mara mbili mpaka tatu kwa wiki, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kujificha katika vinyweleo. Sasa basi kwa mfano mimi mwenyewe Binafsi nina masharti yangu ya kila siku ili kuiweka vizuri ngozi yangu na ndio maana wengi wakikutana LIVE na mimi wananiuliza 'Oooh BEN unatumia nini kwenye ngozi yako? Sasa kwa mfano mimi, kila nikiamka asubuhi lazma ninywe maji glass 2 kabla ya kupiga 'MSWAKI' na mara nyingi mie sinywagi 'CHAI' ila nahakikisha saa 4 ivi napata Juice au 'FRUITS' mchanganyiko tena 'ORIGINO' na sio ya BOX huku mwili wako ukiusindikizia na maji ya kunwa kila baada ya muda flani na pia yakupasa ujue una Ngozi ya aina gani ili utumie 'LOTION' au 'CREAM' ya aina gani yatakayokufaa zaidi mwilini. Alafu hakikisha kila mara unafanya mazoezi na mwili utoke JASHO jingi ili ngozi itoe uchafu kwenye 'VITUNDU! Na pia hakikisha kabla hujalala unakunywa tena Glass 2 za maji na pia ni marufuku kulala na 'MAKE UP' usoni na endapo utaaamka usiku kwenda 'MSALANI' kunywa tena 2, fululiza ivyo kwa wiki 2 utanipa majibu mwenyewe!
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: KWA NGOZI NYORORO YENYE KUWAKA, NISIKILIZE MIMI SASA... Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top