Wengi wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ambazo
nyingine si sahihi sana katika kufanya ili mradi kuwemo na amani akilimi na
kwenye mwili.
Wengi wetu tunataka matumbo yawe wastani hasa yale
ambayo hayajitokezi katika nguo zetu.
Ipo njia ya haraka ya kupunguza tumbo njia hiyo ni
kubadili mfumo wa ulaji.
Unaweza kwa kuanza kula mbogamboga na matunda kwa
wingi na kupunguza kula vyakula vya kukaanga na kufanya mazoezi ya kutembea.
Njia salama
ya kupunguza tumbo ni ile ya kupangilia vyakula, usijinyime kula kwa kudhani
kwa kufanya hivyo unaweza kupunguza tumbo njia hiyo inaweza kuleta madhara
makubwa . Punguza kula vyakula vyenye wanga tumia mboga mboga
na matunda kwa wingi pia punguza vyakula vyenye sukari nyingi.
Vyakula kama viazi mviringo, wali, mkate hukaa
tumboni zaidi ya siku tatu, Unashauriwa kuacha kula nyama nyekundu ambayo
husababisha kuongeza uzito na kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo pia.
Unaweza kuwa unakula vizuri na unafanya mazoezi
lakini ukawa na tatizo hili, kuna wakati tumbo linajitokeza kuliko kawaida.
Mara nyingi hali hii husababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi kama
hunywi maji ya kutosha, kula bila mpangilio maalum au kula mara moja kwa siku.
Kula milo mitatu kwa siku .Kunywa maji mengi angalau lita tatu kwa siku sababu kubwa ya
mtu kuwa na tumbo kubwa ni chakula anachokula.
0 comments:
Post a Comment