Habari Mpya

Friday, 17 January 2014

Michelle Obama to mark 50th birthday on Friday

Washington, USA.

   
Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Washington Post, baadaye mwezi huu First Lady Michelle atatimiza miaka 50 ambapo mwaliko kwa wageni wote uliwashauri kula kabisa kabla hawajaja kwenye tafrija ya kuzaliwa kwake.

IkWageni wote watakao hudhuria hafla ya kusherehekea miaka 50 ya kuzaliwa ya mke wa raisi wa Marekani, Michelle Obama katikaulu ya Marekani (White House) hawatokula chakula cha jioni.

Katika halfa hiyo ya kukata na shoka inayosubiriwa kwa hamu, wageni wametakiwa kujiandaa ipasavyo, viatu visafi kwaajili ya kusakata rumba la ukweli.
Hata hivyo huo umekuwa ni mtihani mkubwa kwa waandaaji wa shughuli hiyo huku wakikuna vichwa jinsi shughuli hiyo itakavyokuwa.
Watu mbali mbali hawakusita kuonyesha hisia zao kutokana na tukio hilo.

“Sidhani kama kuna ubaya, lakini pia ni tofauti kidogo na jinsi watu walivyozoea” alisema Lizzie Post, mjukuu wa mwandishi maarufu wa kitabu cha masuala ya hafla za nyumbani.
Naye rafiki wa karibu wa Oprah Winfrey, Colin Cowie alitoa hisia zake “kuwaambia watu wale kabla hawajaja sivyo ambavyo ningefanya, mara nyingi nafikiri chakula ndio kinawafurahisha watu ikifuatiwa na muziki, bar iliyopendeza na huwezi kuvitenganisha”

Bi Obama alisikika akiwaambia watoto wa shule hivi karibuni kuwa anakaribia kufikia miaka 50 na kwamba atasherehekea ki-namna yake mwenyewe. Na kuamini kwamba jinsi unavyozidi kukua, ndiyo unavyozidi kuwa huru kusema unachotaka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Michelle Obama to mark 50th birthday on Friday Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top