1. Jua unataka nini.
Hili ni jambo la kwanza la msingi ambalo mvaaji anatakiwa
alifikirie kwa ubakini kabla ya kufanya maamuzi ya baadaye. Zingatia
muingiliano wa uhitaji wako na mahali husika wa vazi utakalo vaa. Kwa mfano, je
vazi hilo wataka kulitumia kwenye sherehe, hafla au tafrija za namna gani?
2. jua umbo lako ili kufanya
uchaguzi.
Kitu muhimu cha kuzingatia katika
hili ni namna gani vazi ulilovaa linashabihiana na umbile la mwili wako. Kataa
kabisa kuvaa nguo ambazo ni aidha zinakubana sajna au oversize ya mwili wako
kwani hii yaweza kutoa taswira tata mbele ya wanajamii.
3.Chagua Rangi.
Hapa waweza kuchagua rangi yoyote
uipendayo kutokana na jinsi ya utashi wako unavyokutuma. Kama wewe ni mtu
maarufu na unataka pengine watu wafahamu uwpo wako katika tukio Fulani basi
crazy colours zinakufaa kama vile njano, nyekundu na blue .
4.Staili ya mavazi
Majarida, vipeperushi na mitandao ya
tovuti ni sehemu nzuri za kufahamu mitindo mbali mbali ya mavazi. Amka na acha
tabia ya kukariri mitindo ya mwaka 47, kumbuka vazi utakalovaa litakuwa ni
ukumbusho wako kwa vizaji vijavyo.
5.Duka la Mavazi
Kumekuwa na ushindani mkubwa sana
siku hizi katika ushindani wa maduka ya mavazi hususani nchini Tanzania nahii
inakupa mwanya mkubwa kwa wewe mvaaji kuchagua bidhaa bora na kwa bei nafuu.
Tambua kuwa vazi zuri si lazima liwe ni lile la gharama za juu peke yake bali
hata yale mavazi utakayo nunua kwa wamachinga yanaweza kukutoa vizuri na
ukapendeza
6.Pambo za ziada (accesories).
Ili mvaaji aweze kungara zaidi
atokapo na vazi lake mara njingi tunashauriwa kuwa na chaguzi sahihi za mapambo
ya ziada yanayoendana na kile tulichokivaa kama vile heleni, mikufu,
mikoba, saa za mikononi, miwani, mitindo ya nywele na mengineyo yafananayo na
hayo.
0 comments:
Post a Comment