Habari Mpya

Wednesday, 25 November 2015

MIEZI NANE YA MIMBA YA KARDASHIAN NI MATATAMwanamama mwenye umri wa miaka 35 Kim Kardashian, ambaye anajishughulisha sana na mitindo kwa sasa amebakisha mwezi mmoja kuweza kupata mtoto wa pili amesema ameamua kuacha kwa muda mambo ya fasheni kutokana na mabadiliko ya mwili wake
“ni ngumu kuweza kufuatilia mitindo “ kim Kardashian alisema wakati akiongea na mwanamitindo mwenzake Guru Andre Leon Talle katika uzinduzi wa  jarida jipya la Vorgue, Kim aliendelea kusema kuwa “marafiki zangu wananishangaa na kusema nimeamua kuachana na mitindo na mimi nawajibu kwanini na kwa nini unasema hivyo lakini wanasema unavaa kawaida wamekuwa wakiniona katika picha tofauti ninazopiga kwa sasa”
Aidha si kawaida kwa Kim kwani amekuwa akilalamikia sana kuhusu miguu yake kujaa na kushindwa kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu, huku akicheka alisema " imefikia wakati sasa miguu yangu imekuwa ikijaa ingawa sio kama ilivyokuwa mwanzo lakini ndio ipo hivyo kwakweli nipo mwishoni kwa kuwa na hali hii naamini siku itafika na nitarudi katika hali yangu ya kawaida katika mitindo”
Hata hivyo mimba yake haimzuii kufanya mpangilio mzuri wa chakula chake cha kila siku hivyo amekuwa akifuatilia ulaji wake kwa kuzingatia milo yote mitatu katika ubora hasa katika hali aliyonayo
“kila asubuhi nakula mayai meupe na maparachichi, pia uji lakini kwa mchana napenda salad na usiku nakuala risotto au tambi”.alisema Kardashian
Kimkardashian sio mpenzi sana na kutoa shukrani ya chakula lakini amebainisha kutakuwa na zoezi hilo mwaka huu nyumbani kwa mama yake Kris Jenner hapo ndipo anapoona mabadiliko na kipindi baba yake alipowazoesha kufanya shukrani hizo kipindi cha nyuma
“kila tunapotoa shukrani huwa  mapumziko na baba yangu lakini kwa sasa tunaenda kwa ndugu tofauti mfano nyumbani kwa dada yangu hii ni mabadiliko ya kimila” alisema Kardashian
 
Mwanamama huyo amebakisha mwezi mmoja kuweza kupokea mtoto mwingine baada ya North West ambaye atamkaribisha mdogowake toka kwa mama yake huyo, anayezaa na mwanamuziki Kanye West
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: MIEZI NANE YA MIMBA YA KARDASHIAN NI MATATA Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top