Habari Mpya

Friday 13 February 2015

NJEGERE ZA MAZIWA.


Njegere Ni chakula cha kawaida kabisa kwa watanzania wengi. njegere hizi hutumika kwa milo tofauti ya siku ukipenda



Njegere zina namna tofauti pia hata katika mapishi yake na hii ni moja ya namna ya kuandaa njegere kama sehemu ya mlo mkuu.


katika namna ya upishi wa leo kumetumika Beef masala kama moja ya kiungo.Ingawa kiungo hiki ni maalum kwa nyama,kinaleta ladha nzuri sana kwenye Njegere.unachotakiwa kujua mwenzangu upishi ni sanaa usikariri shughulisha almashauri yako ya kichwa upike chakula kitakachowapendeza walaji wako.






Mahitaji
Njegere ½ kilo
Nyanya 3 kubwa
Swaumu ½ kijiko cha chai
Beef Masala kijiko 1 cha chai
Nyanya ya Kopo vijiko 2 vya chai
Maziwa fresh kikombe 1 ½
Karoti Mbili,kata duara
Mafuta vijiko 4 vya chakula
Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha njegere adi ziive,ziwe laini na Maji yakauke.
2.Katika sufuria unga mafuta na kitunguu adi kitunguu kianze kubadilika rangi(usiache kikawa cha brown) ,Ongeza nyanya,nyanya ya kopo,chumvi,swaumu na beef masala.Kaanga adi nyanya na mafuta zitengene ndani ya sufuria.
3.Ongeza njegere na karoti ,kaanga kwa pamoja adi njegere na nyanya zishikane.Ongeza maziwa,chemsha uku unageuza mara kwa mara ili maziwa yasikatike na yasiungulie chini.Chemsha adi upate uzito unaopenda.Tayari kwa kula. Basi tukutane tena hapahapa wakati mwingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: NJEGERE ZA MAZIWA. Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top