Habari Mpya

Friday, 13 February 2015


Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto Nasra Rashid (mtoto wa box) akifikishwa mahakamani kwa kusomewa shtaka lake upyaaaa, mahakama ikafuta mashtaka ya kwanza yaani kula njama na unyanyasaji mpaka kesi ya mauaji

 poli kila mahala wakihakikisha watuhumiwa hawa hawachomoki kamwe
 wakazi wa mkoa wa morogoro nao hawakuwa nyuma nia ni kujua hawa mwenzetu wanaishia wapi na kesi yake hiyo, iliyo pelekea kuudhalilisha Mkoa wa Morogoro

 

 

 JIACHIE NA JEZI RASMI ZA TIMU ZOTE 32 ZINAZOKWENDA BRAZIL

Kama upo au unaishi katika miji mikubwa duniani[na pengine hata ile midogo] bila shaka utakuwa umeshaanza kuona watu wakiwa wamening’iniza bendera mbalimbali iwe katika nyumba zao au magari. Wengine wameshaanza kuvalia jezi mbalimbali za mataifa yao au yale wanayoyapigia upatu. Ni kwamba muda wa mashindano maarufu ya fainali za Kombe la Dunia 2014[FIFA World Cup 2014] ndio yapo pua na mdomo.
Endapo na wewe una mpango wa kuwa mshabiki wa ndani zaidi,hizi hapa ndizo jezi rasmi za timu zote zinazoteremka dimbani huko Brazil kuanzia June 12 mpaka July 13. Mimi nimeshachukua Brazil kwa upande wa dunia na Ghana kwa upande wa Afrika.Wewe je?
WorldCup2014Kits

 

KAMA ULIKUA HUJUI HIVI NDIVYO VIWANJA 12 VITAKAVYOWAKA MOTO NCHINI BRAZIL KUANZIA TAREHE 12 JUNE -13 JULY 2014[PHOTOS]

Maandalizi ya viwanja ni miongoni mwa mambo muhimu sana wakati wa maandalizi ya mashindano makubwa kama ya Kombe La Dunia la Soka. Kuna vinavyofanyiwa marekebisho tu [renovation] na kuna vinavyojengwa kuanzia chini kabisa [brand new stadiums]. Yote ni kuhakikisha usalama wa mashabiki[security] na pia ubora wa mchezo wenyewe…The Beautiful Game of Soccer.
Pamoja na kwamba Brazil wamekuwa wakilaumiwa kwa kutokwenda na wakati katika maandalizi hususani ya viwanja,[tayari wafanyakazi kadhaa wamepoteza maisha wakati wa ujenzi], viwanja hivi 12 vinatarajiwa kuwa tayari kabisa kunako tarehe 12 June ili kusindikiza mpango mzima wa FIFA World Cup Brazil 2014. Jumla ya mechi 64 zinatarajiwa kupigwa mwaka huu.
Ujenzi au ukarabati wa viwanja hivi umedhaminiwa na Brazil Development Bank. Mojawapo ya masharti waliyoweka wadhamini hawa ni kuhakikisha kwamba kila kiwanja kinakuwa cha “kijani” kwa maana ya kuzingatia masuala yote ya utunzaji mazingira. Kila uwanja lazima upate cheti cha LEED [Leadership in Energy and Environmental Design] ambacho kinatambulika kimataifa na ambacho hutolewa na shirika lisilo la kiserikali la  CBG (Green Building Council) Picha hizi hapa.
Belo-Horizonte1
Unajulikana kama Estádio Governador Magalhães Pinto. Una uwezo wa kuingiza watu 62,500. Upo katika jiji/mji wa Belo Horizonte, Minas Gerais. Jumla ya mechi 6 zitapigwa katika uwanja huu.
Brasilia
Jina kamili la uwanja huu ni Estádio Nacional Mané Garrincha. Una uwezo wa kupakia jumla ya watu 71,000. Upo katika jiji la Brasilia, DF (Federal District). Ni miongoni mwa viwanja vipya kabisa vilivyojengwa maalumu kwa World Cup.Jumla ya mechi 4 zitapigiwa hapa ikiwemo ya Brazil  na Cameroon tarehe 23/6.
Cuiaba
Huu unaitwa Arena Multiuso Governador José Fragelli. Upo jijini Cuiabá, Mato Grosso. Unachukua jumla ya watazamaji 42,900. Jumla ya mechi 4 zitapigiwa hapo. Ni mpya.
Curitiba
Jina kamili ni Estádio Joaquim Américo Guimarães. Watu 43,000 wanaweza kuingia kwa mkupuo. Jumla ya mechi 4 zitapigwa hapa. Upo  Curitiba, Paraná.
Fortaleza
Jina kamili la uwanja huu ni Estádio Governador Plácido Aderaldo Castelo. Una uwezo wa kuingiza jumla ya mashabiki 64,800. Upo  Fortaleza, Ceará. Uwanja huu ndio ulikuwa wa kwanza kukamilika katika maandalizi ya fainali za mwaka huu. Mechi 6 zitapigwa hapa ikiwemo ya wenyeji Brazil dhidi ya Mexico tarehe 17/6 na Germany dhidi ya Ghana tarehe 21/6.
Manaus
Uwanja huu ambao dizaini yake ni kama kikapu unaitwa Arena da Amazônia. Una uwezo wa kubeba mashabiki 42,300. Upo jijini  Manaus, Amazonas. Ni miongini mwa viwanja vipya maalumu kabisa kwa fainali za mwaka huu.Mechi 4 zitapigwa hapa ikiwemo ya England dhidi ya Italy tarehe 14/6 na Marekani dhidi ya Ureno tarehe 22/6.

Natal 
Complexo Arena das Dunas upo Natal,  Rio Grande do Norte. Una uwezo wa kuingiza mashabiki 42,000.Mechi 4 zitapigiwa hapa ikiwemo ya Ghana Vs USA tarehe 16/6.
beirario
beira-rio1
Huu unaitwa Estádio José Pinheiro Borda. Una uwezo wa kuingiza watu 56,000 na upo  Porto Alegre, Rio Grande do Sul.Ndio uwanja mkubwa kushinda vingine vyote kusini mwa Brazil. Mechi 5 zitapigwa hapa ikiwemo ya Nigeria dhidi ya Argentina tarehe 25/6.
Recife
Jina kamili la uwanja huu ni Itaipava Arena Pernambuco. Una uwezo wa kuchukua jumla ya watu 46,000. Mechi 5 zitapigiwa hapa. Upo katika viunga vya Recife, Pernambuco.
Rio
Hii ndio Maracana. Jina lake kamili ni Estádio Jornalista Mário Filho. Ndio uwanja wa nyumbani wa timu za Flamengo and Fluminense. Hapa ndipo itakapopigwa fainali ya mwaka huu ikiwa ni mara ya pili kwa uwanja huu kuwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la Dunia. Una uwezo wa kuingiza watu 78,000 na jumla ya mechi 7 zitapigwa hapa. Upo katika jiji maarufu la Rio de Janeiro.
Salvador
Jina la huu uwanja ni refu kidogo.Unaitwa Complexo Esportivo Cultural Professor Octávio Mangabeira / Itaipava Arena Fonte Nova. Jumla ya mashabiki 55,000 wanaweza kuingia uwanjani hapa kwa raha mustarehe.Upo katika jiji la Salvador, Bahia. Mechi 6 zitapigwa hapa ikiwemo ile ya Spain dhidi ya Netherlands tarehe 13/6. Kama utakumbuka Spain na Netherlands ndio waliingia fainali mwaka 2010 kule Afrika Kusini na Spain kuibuka Bingwa wa Dunia kwa ushindi wa goli 1-0.
I_QAjCQJ_lzlTpN6RXr8mN7tJbsk1j1dH2r6oX3P3PI
Arena de São Paulo / Arena Corinthians upo jijini Sao Paolo. Una uwezo wa kuchukua mashabiki 65,800. Hapa ndipo mechi ya ufunguzi itakapofanyikia. Ni kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia tarehe 12/6.

WAZIRI CHIKAWE AUNGANA NA MAAFISAWAKE KUSHANGILIA KUPITISHWA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, BUNGENI DODOMA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea pongezi kutoka kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) mara baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuipitisha Bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) kwa kuyajibu kwa ufasaha baadhi ya maswali ya Waheshimiwa Wabunge na hatimaye Bajeti ya wizara hiyo ya Mwaka wa Fedha 2014/15 kupita. Kulia kwa Naibu Waziri Silima ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimfafanulia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, jinsi alivyoyajibu maswali ya waheshimiwa wabunge kabla ya kupitishwa Bajeti ya wizara hiyo ya Mwaka wa Fedha 2014/15. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) wakipongezana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima kwa kuyajibu maswali mbalimbali ya waheshimiwa wabunge na hatimaye Bajeti ya wizara yao kupitishwa na Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Nyuma yao, Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

RAIS SHEIN AMKARIBISHA IKULU YA ZANZIBAR WAZIRI CHIKAWE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar leo.  Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.  (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (watatu kushoto), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima (wapili kulia), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dickson Maimu (wapili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa, Ofisi ya Zanzibar, Vuai Suleiman. Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame. Waziri Chikawe alifika Ikulu ya Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais Shein baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.  (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

 

Masood Kipanya 

 

Zitto aibuka kidedea mahakamaniWafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto na wale wa uongozi wa juu, jana walipambana tena mahakamani kwa ngumi na mawe kisha kusababisha watu wawili kujeruhiwa.PICHA|MAKTABA  

Kwa ufupi
Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya sheria, kanuni, amri na uamuzi wa kesi mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na za nje, Jaji Utamwa alisema anakubaliana mtoa maombi.


Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameshinda maombi yake dhidi ya chama hicho mahakamani.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, aliiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kuizua Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake.
Zitto kupitia kwa Wakili Albert Msando alikuwa akiiomba Mahakama itoe zuio hilo la muda hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Katika uamuzi wake jana, Mahakama Kuu ilikubaliana na maombi na hoja za Zitto na kutoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema na au chombo chake chochote cha uamuzi kumjadili na kutoa uamuzi wowote kuhusiana na uanachama wake, hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Awali, Mawakili wa Chadema wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi matakwa ya kupewa zuio la muda.
Katika uamuzi wake, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa maombi hayo yametimiza matakwa yote ya kupewa zuio hilo.
Matakwa hayo ni pamoja na kuwapo kwa mgogoro baina ya pande mbili, hasara au madhara yasiyoweza kufidiwa na usawa katika athari kwa pande zote.
Jaji Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Msando kuwa iwapo Mahakama haitaingilia kati na kutoa zuio hilo, mtoa maombi ataathirika zaidi kuliko wajibu maombi.
Akijibu hoja ya Wakili Lissu aliyepinga hoja ya mtoa maombi kuathirika pamoja na wananchi wa jimbo lake kwa kukosa uwakilishi bungeni, kuwa hata akipoteza ubunge kwa kuvuliwa uanachama utaitishwa uchaguzi mdogo, Jaji Utamwa alisema uchaguzi mdogo huwa unachukua mchakato mrefu.
Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya sheria, kanuni, amri na uamuzi wa kesi mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na za nje, Jaji Utamwa alisema anakubaliana mtoa maombi.
“Kwa hiyo ninatoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chadema na au chombo chake chochote cha uamuzi kwamba kisimjadili na kutoa uamuzi wowote dhidi ya mleta maombi kuhusiana na uanachama wake kusubiri kusikilizwa na kuamuriwa kwa kesi yake ya msingi,” alisema Jaji Utamwa.
Kabla ya kufikia uamuzi huo, Jaji Utamwa alitupilia mbali hati ya kiapo kinzani ya Chadema iliyotolewa na Wakili Kibatala baada ya kuwekewa pingamizi na Wakili Msando ambaye alidai kuwa katika hati hiyo, kuna taarifa za kusikia ambazo hakueleza alipozitoa.

Huku akirejea vifungu vya sheria, kanuni, amri na uamuzi wa Mahakama mbalimbali, alisisitiza kuwa ingawa wakili anaweza kuapa kwa niaba ya mteja wake, lakini anapaswa kueleza chanzo cha taarifa anazozitoa katika kiapo hicho.
Baada ya kutupilia mbali kiapo hicho, Jaji Utamwa alisema hata vielelezo vya wajibu maombi vinakufa kifo cha kawaida na kwa hali hiyo, maombi ya mtoa maombi yanabaki bila kupingwa na kwamba hakuna haja pia ya kujadili hoja za upande wa wajibu maombi.
Baada ya Jaji kutoa uamuzi huo, Zitto, aliwafuata mawakili wa Chadema na kupeana nao mikono kisha akaongozwa na walinzi wake kutoka nje ya Ukumbi wa Mahakama akipitia mlango maalumu unaotumiwa na jaji.
Kabla ya hukumu
Zitto aliyekuwa amevalia suti ya kijivu na shati la michirizi myeupe na ya kijivu aliwasili mahakamani hapo saa 7:45 mchana akiongozana na walinzi wake binafsi (mabaunsa), wapambe na wakili wake.
Baada ya kufika alikwenda katika chumba maalumu ambako alipumzika hadi saa 9:45 alasiri alipoingia katika ukumbi na kukaa katikati ya wapambe wake huku nyuma yake wakiwapo walinzi wake.
Jaji Utamwa aliingia mahakamani saa 9:56 alasiri na kuanza kusoma uamuzi wake akianzia na pingamizi la Zitto kwenye hati ya kiapo kinzani cha Chadema kisha akamalizia na uamuzi wa maombi ya msingi. Hukumu hiyo ilimalizika kusomwa saa 11:10 jioni.
Baada ya hukumu
Akizungumza baada ya uamuzi huo, Wakili Msando alisema wameupokea kwa furaha uamuzi huo wa mahakama na kwamba hiyo ni hatua mojawapo ya haki akisema anaamini kuwa mteja wake atapata haki anayoitafuta.
Hata hivyo, Lissu na Kibatala kwa nyakati tofauti walisema kuwa ingawa wanakubaliana na uamuzi huo, hajawaridhika.
Maombi hayo ya Zitto yaliyotolewa uamuzi jana yanatokana na kesi ya msingi aliyofungua mahakamani hapo Januari 2, mwaka huu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema.
Katika kesi hiyo anaiomba Mahakama izuie chama hicho, wakala wake na vyombo vyake vya uamuzi kumchukulia hatua zozote wala kumjadili kuhusiana na uanachama wake, hadi hapo rufaa anayokusudia kuikata Baraza Kuu la Chadema kupinga kuvuliwa nyadhifa zake itakaposikilizwa.

Kesi hiyo ya msingi imepangwa kutajwa Februari 13, 2014.
Mapambano tena
Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto na wale wa uongozi wa juu, jana walipambana tena mahakamani kwa ngumi na mawe kisha kusababisha watu wawili kujeruhiwa.
Vurugu hizo zilitokea saa 7.55 mchana muda mfupi baada ya Zitto kuingia mahakamani.
Katika vurugu hizo, mmoja wa wafuasi hao ambaye jina lake halikujulikana mara moja, aliumizwa kichwani baada ya kupigwa na jiwe na mwingine alipigwa jiwe tumboni na kupelekwa hospitali.
Kutokana na vurugu hizo, polisi waliyatenganisha makundi hayo katika sehemu tofauti na kukaa katikati ili kuyatenganisha.
Wakati Zitto akiwasili mahakama hapo, wafuasi wake walikuwa wakiimba `Zitto Zitto kama Mandela’ hali iliyowalazimu wafanyakazi wa Mahakama kuingilia kati na kuwazuia.
Makundi hayo ya wafuasi wa chama hicho yalifika mapema saa 6:30 mchana mahakamani hapo kusikiliza uamuzi uamuzi wake.
Ulinzi katika eneo lote la Mahakama uliimarishwa, makundi ya polisi wa kawaida na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi walitanda sambamba na askari wa kikosi cha mbwa, magari manane ya polisi na matatu ya maji ya kuwasha.
Kama ilivyokuwa juzi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha Mahakama.
Baada ya mahakama kutangaza uamuzi wake, wafuasi wa Zitto walishangilia kwa nguvu na kuondoka wakiimba nyimbo za kumsifu kiongozi huyo.
Mtei amwonyesha mlango Zitto

Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.
Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.
Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida... “Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.”
Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho.
IGP MPYA AKUTANA RASMI NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JANA, WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA JESHI LA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto) akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto) kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Tatyana Celestine, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu baada ya mazungumzo yao kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Tatyana Celestine, Wizara ya Mambo ya Ndani.

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top