Habari Mpya

Tuesday 27 May 2014

Tanzania-New York based model Millen Magese,Oparation 10 na mbili kati ya hizo alifanyia Marekani.



.

Tanzania-New York based model Millen Magese, ambaye alishinda taji  la Miss Tanzania na kuiwakilisa nchi katika mashindano ya Miss world nchini Afrika kusini, alizaliwa tar 22 September 1982

Leo amekuja kuhamasisha wanawake kufahamu tatizo linalomkabili mpaka kupelekea kuwa gumu katika maisha yake ingawa anajitahidi kulikubali, Millen anasema hakuna mwanamke asiyependa kuwa mama lakini endapo utakumbwa na tatizo kama la kwake kuna njia nyingine ambazo zinaweza kumsaidia mwanamke asiwe mpweke kwa kukosa mtoto, kuna njia ya kupandikiza mayai, kuna njia ya kupandikiza mayai yako kwa mwanamke mwingine lakini pia kuna njia ya kurithi watoto na ukajiskia kama mwanamke mwingine ambaye ni mama.

Imekuwa kawaida kwa wanawake wafikapo katika siku zao za hedhi kuumwa tumbo na kuona ni kawaida, millen happiness magese anasema kuumwa tumbo ni kawaida lakini usiumwe kupitiliza hilo ni tatizo, "endapo utaumwa na kulazwa, kutapika sana, kuchoma sindano tambua unatatizo hiyo si hali ya kawaida" imekuwa kawaida kwake kipindi chote alichokua akisoma kuugua kwa kupitiliza na ikifika wakati katika maisha yake ya shule kufanya kitu fulani na wenzake kugundua ataumwa kunabaki pengo kubwa na katika team hiyo kunaonekana upungufu " ilifika wakati hata tukiwa tunasafiri kuelekea katika michezo na nikiwa naumwa basi lazima inafika mahala gari itasimama na mie ntatolewa nje kwa ajili ya kuchoma sindano ndipo ntajiskia vema, na hii imenipelekea nikawa najichoma sindano mwenyewe".
Ni tatizo alilodumu nalo tangu akiwa shuleni bila kufahamu anaugua nini lakini baada ya kukutana na Jane ambaye amekua mtu wakaribu sana katika maisha yake hasa kipindi alipofika south afrika na kumwona anafaa kuingia katika mambo ya modeling akamuamini na ndipo akawa mlezi wake wa karibu marazote alipokuwa akiumwa, tangu afahamike na tatizo hilo amekwishafanya oparation 10 na mbili kati ya hizo alifanyia Marekani.
Imefikia wakati Tanzania ianzishe Hospitali ya wanawake ili kuwalinda na kuwajali kwani wanawake wakijaliwa ni rahisi kuwa na familia bora na zenye afya njema, Millen akusita kutoa shukrani zake nyingi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumpokea na kumsiliza jambo lake pia kusema ni jambo zuri ambalo kila mtanzania anatakiwa kufahamu, mambo ya uzazi nchini yamekuwa yakifichwa fichwa kutokana na utamaduni wetu lakini endapo matatizo yakifichwa basi tunapelekea matatizo kukua wakati njia zipo za kuweza kuwasaidia watu kuepukana na matatizo.
 
Ni mmoja ya wanawake wanaojitoa kusaidia wengine kutambua na kushughulikia  tatizo hili kabla ya  halijawa  kubwa kushindwa kutibika kama ilivyo kuwa kwake, hivyo yupo tanzania kwa ajili hiyo
 Fashion Time na Tatyana Celestine blogspot inaunga mkono kwa asilimia mia kufanikisha zoezi hilo  hapa Tanzania wote tujumuike pale Cocobeach siku ya jumapili kuweza kusikia nini hasa kinamsumbua Millen Magese pia kujua njia ambazo zinaweza kukusaidia kuhepuka tatizo hilo.
 
 Ama kwa hakika kwa majina aliwaita watu maharufu kama Wema Sepetu, Diamond Platnum, Faraja Kota, Lady Jay Dee na wengine wengi ili kusaidia kufanikisha kufahamisha jamii kuhusu tatizo hili ambalo kwake ni maumivu na limemsumbua kwa muda mrefu.


 
 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Tanzania-New York based model Millen Magese,Oparation 10 na mbili kati ya hizo alifanyia Marekani. Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top