Habari Mpya

Thursday 13 March 2014

NYERERE AIBUA HOJA NZITO ATAKA SERIKALI IMKAMATE MREMBO AGNESS GERALD a.k.a MASOGANGE JUU YA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA.

Agnes Gerald ‘Masogange’. 

WAZIRI Kivuli wa Mambo ya Ndani, Vincent Nyerere ameibuka na kutoa kauli ya kutaka Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ akamatwe na kuswekwa ndani akidai kitendo cha kuachiwa huru Afrika Kusini kwa kesi ya madawa ya kulevya si sahihi kwa Tanzania.
Akizungumza na Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani Jumatatu usiku na Runinga ya ITV, Nyerere alisema baada ya uchunguzi kufanyika ilibainika kuwa yale madawa kwa nchini Afrika Kusini si ya kulevya lakini kwa Tanzania ni ya kulevya.


Alisema kutokana na kubainika kwamba yalitokea nchini, baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar walitimuliwa kazi, akasema basi ilikuwa lazima Masogange baada ya kutua Tanzania akamatwe.
 


“Mimi nimeshangaa sana jamani, ilikuwaje watu watimuliwe kazini pale uwanja wa ndege kwa kuwatuhumu kuruhusu madawa ya kulevya kupita, kwa nini walimuachia huru yule binti (Masogange), basi waliofukuzwa nao warudishwe kazini,” alisema Nyerere.


Paparazi wetu, juzi alifanya jitihada za kuzungumza na Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe lakini simu yake ilikuwa ikiita tu.


Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa alipopigiwa simu alisema kule Afrika Kusini Masogange alipatikana na hatia na kuhumumiwa, kwa hiyo hakuna sheria ya kumkamata tena hapa nchini.


“Kule alihukumiwa kwenda jela au kulipa faini, ina maana alipatikana na hatia, akalipa faini na kuachiwa, sasa kwa nini tumkamate huku?” alihoji Nzowa.
Simu ya Masogenge juzi ilikuwa ikiita mara kadhaa bila kupokelewa.


Julai 5, mwaka jana, Masogange na Melisa Edward walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Kesi yao iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo ambapo Masogange alikutwa na hatia na kuhukumiwa kwenda jela miezi 32 au faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru baada ya kuonekana hakuwa na hatia. http://jijiletutz.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: NYERERE AIBUA HOJA NZITO ATAKA SERIKALI IMKAMATE MREMBO AGNESS GERALD a.k.a MASOGANGE JUU YA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA. Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top