Habari Mpya

Monday, 3 March 2014

Kitu muhimu ambacho kinaweza kukuonyesha kuwa wewe ni mrembo au la ni......


Kitu  muhimu ambacho kinaweza kukuonyesha kuwa wewe ni mrembo au la ni namna unavyotunza meno yako.

Kama meno yako ni machafu au hayana weupe wa kutosha huwezi kujiita mrembo unatakiwa kutengeneza suala hilo. Kitu cha muhimu kwa utunzaji wa meno ni kuhakikisha angalau unapiga mswaki mara mbili kwa siku, hapa namaanisha asubuhi na jioni. Njia nyingine ya kuwa mrembo ni kufahamu namna ya kujipamba uso wako.

Unatakiwa ufahamu poda maalum kwa ajili ya ngozi yako, unapokwenda dukani kununua poda hakikisha unalinganisha ngozi yako na poda husika.

Tafuta ‘moisturizer’, ambayo ni nzuri, pendelea kutumia mascara, kama unapenda ‘lip stick’ basi pendelea kupaka ya pinki lakini ambayo haijaiva sana. Pendelea kufanya ‘scrub’ kwa ajili ya ngozi yako ya mwili mzima, fanya ‘scrub’ angalau mara moja kwa wiki, hiyo itasaidia kuondoa ngozi iliyokufa na kukufanya ung’ae.

Mazoezi ni njia nzuri ya kukufanya uonekane mrembo. Kama unajihusisha na mazoezi maana yake ni kwamba huwezi kuwa na uzito mkubwa.

jipe muda wa kupata usingizi wa kutosha, kama hulali vizuri uso wako utachoka mapema na wakati mwingine unaweza kupata mikunjo ya uzee mapema. Kula mlo kamili, hakikisha hukosi mboga za majani na matunda kila siku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Kitu muhimu ambacho kinaweza kukuonyesha kuwa wewe ni mrembo au la ni...... Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top