Habari Mpya

Saturday, 15 March 2014

‘Hydroquinone’ na ‘Mercury ’ Kemikali hatari, ni bidhaa zinazotumika kujichubua


.

Imekua kawaida kwa karne ya sasa wanawake wengi kufikiri kuwa mweupe ndio urembo.
Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
 Na hii imepelekea Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua
Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.
 
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa tu tena maelekezo ya daktari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: ‘Hydroquinone’ na ‘Mercury ’ Kemikali hatari, ni bidhaa zinazotumika kujichubua Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top