Miss Universe Tanzania, Betty Boniface amesema pamoja na kutofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora Miss Universe Dunia, anajivunia kutangaza utalii wa Tanzania.
Miss Universe, Betty alikuwa Russia kwenye
mashindano ya Miss Universe dunia yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu
na Maria Gabriela Isler wa Venezuela kunyakuwa taji la Miss Universe
2013.
Betty aliyeng’ara katika vazi la Taifa kwa kuvaa
vazi la mkeka lililobuniwa na mbunifu chipukizi, Mwanakombo Salim kwa
kusaidiana na wasanii wa Tingatinga, alisema kuwa pamoja na kutofanikiwa
kuingia hatua ya 16 bora, anachojivunia ni kuitangaza nchi kwa kupitia
vivutio vya utalii akiwa balozi wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) ambao
walikuwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Universe Tanzania.
Alisema katika mashindano hayo alikuwa mrembo pekee kutoka bara
la Afrika aliyechaguliwa miongoni mwa warembo nane kote ulimwenguni
kushiriki katika kipindi maarufu mjini Moscow kinachoonyeshwa duniani
kote kijulikanacho kama “Let Them Talk” kinachoendeshwa na mtangazaji
maarufu Andrey Malakhov.
Betty alisema kuwa katika kipindi hicho ambacho
kinapatikana kwenye mtandao, alionekana kuwafurahisha sana hadhara ya
warusi katika studio na kusifiwa kwa kuwa mrembo wa kipekee na mwonekano
wake wa kiafrika.
Alifafanua kuwa baadhi ya majaji wa mashindano ya
Miss Universe walikuwepo na walieleza kuvutiwa na Betty na kumwona kama
mrembo ambaye alikuwa ana nafasi kubwa ya kuingia 16 bora.
“Kipindi chote nilipokuwa Russia, niliona
kukubalika na Warussia wenyewe na hata vyombo vya habari vya kimataifa.
Nina furaha kubwa sana kwani kilichonileta nimekifanikisha kwani lengo
langu kubwa zaidi ya ushindi ilikuwa ni kuhakikisha naitangaza vyema
Tanzania na vivutio vyake, kama vile hifadhi za taifa za Ruaha,
Udzungwa, Katavi na mengineyo” alisema Betty.
Alisema kuwa kwa msaada mkubwa wa ubalozi wa
Tanzania nchini Russia, alifanikiwa kufanya mahojiano na gazeti maarufu
la utalii nchini humo lijulikanalo “Hot Line travel Magazine.
chanzo: Mwananchi
chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment