Monday, 9 December 2013

MAVAZI YANACHOCHEA MAHUSIANO KATIKA JAMII

 

Mavazi ni kitu pekee katika maisha ya mwanadamu ambayo kwa namna moja ama nyingine huongeza mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume hasa watu wanapokuwa katika uchumba kabla ya kuingia katika mahusiano ya ndoa kama mke na mume

Mwanaume naye huwa ana nafasi yake kwa mwanamke ambapo wanawake wa kisasa wanataka mvulana ambaye yupo (smart) msafi na mtu wa kupangilia nguo zake wakati anapotaka kutoka kwenda kazini ama siku ya kupumzika ambapo lazima uwe na mavazi ya siku ambazo huendi kazini


Kwa mfano unapovaa suruali ambayo inaendana na mwili wako rangi ya kiatu iwe sawa na mkanda wa kiunoni na hapo ukiwa umenyoa vizuri ndevu zako na kutengeneza vizuri nywele zako ambapo wanawake wengi wa dunia hii ya sasa wanapenda wanaume ambao ni wasafi na wenye kupangilia mavazi yao kulingana na jinsi walivyo

Mwanaume yeyote anayejua kupangilia mavazi yake hupendwa na wanawake wengi hata kama hana pesa lakini mwanamke huwa tayari kuwa naye na kusaidia katika maisha na si kwamba wanafuata uzuri walionao kwa maana ya (handsome)

Wanawake huathirika kisaikolojia kwa kumuona mwanaume msafi na anayependa kumuona mchumba wake akiwa amependeza kwa kuvaa mavazi ambayo yanaendana na mwili wake ambapo yanakuwa sio makubwa hata kama mwili wako ni mdogo unapojijua uvae mavazi ya aina gani unapendeza basi hilo linakuwa sio tatizo  kwa mwanamke kujisifia kwa wenzake kuwa mchumba wake ni kijana anayekwenda na wakati

Mavazi yanaweza kukutambulisha wewe ni mtu wa namna gani katika jamii ikiwemo na tabia zako kulingana na jinsi unavyovaa katika mazingira unayoishi ama unayofanyia kazi ambapo kwa sasa Nchini Tanzania ni Marufuku kuvaa suruali ya jinsi wakati wa siku za kazi katika ofisi za serikali na baadhi ya ofisi za watu binafsi

mavazi yanaweza kumfikisha mwanamke mbali zaidi na kile ambacho  mwanaume anacho na amechagua kuvaa zaidi ya kile kuangalia kama na kuona kama uso unaweza kupotosha kutokana na mavazi ambayo ameyavaa  Watu wanaweza kuangalia kama wewe ni mchumba halisi na kugeuka kutoka kuwa wajinga ambapo  wanaweza kuangalia na kugeuka kutoka kuwa kweli tamu, mkali, kuvutia watu.


Kwa kupitia mavazi tu mwanamke anaweza kukupenda kulingana  na jinsi unavyopangilia mambo yako katika kuvaa kwa kuangalia uko katika mazingira gani ya hali ya hewa ya baridi ,joto ama ya kawaida kulingana na mahali ambapo mtu yupo


Wapo watu duniani wanatambulika kutokana na mavazi yao na kila kitu duniani kinatambulika kwa mavazi na nembo zao ambapo kwa mfano wa askari wa Tanzania mavazi yake ni tofauti na askari wa marekani ama uingereza ambapo mwanamitindo utamjua kwa mavazi yake mfanyakazi wa kiwandani nao mwanavazi yao tena wengine wana kofia zikiwatambulisha kuwa ni watu wa sehemu fulani

Waarabu utawajua kwa mavazi yao,lakini nchi ambayo mavazi yake yanapewa heshima ulimwenguni kote ni uvaaji wa nchi za Kimagharibi ambapo vazi la suti huwa linapewa sheshima karibu kila sehemu likiwemo la kuvaa shati lenye rangi moja yaani (plain)


Msichana mmoja alipoulizwa kuwa amempendea nini mchumba wake alisema kinachomfanya ajisikie kuwa naye ni vile anavyovaa na navyopangilia nguo zake sihitaji pesa zake maana hata ndugu zangu wakimuona huniuliza umempataje kijana nayevaa vizuri na wakati mwingine huwa wananione wivu kwani na wao huwalazimisha wachumba wao wawe kama wa kwake

Yapo mavazi ambayo unatakiwa kuvaa kulingana na wakati kwa mfano aliyekuwa raisi Rais wa Libya marehemu Muamar Ghadafi ambapo kitu kikubwa kilichomfanya ajulukane zaidi ni staili yake ya mavazi kila alipokuwa akienda na  katika picha uya pamoja na viongozi wenzake  utamuona mara moja kwa kuwa yeye alikuwa havai suti kama viongozi wengi wanavyovaa katika mikutano

Mavazi pia kukufanya upate marafiki wengi ndani na nje ya nchi kulingana na kazi unayoifanya ambapo unaweza kuwa kinara ofisini kwa upangiliaji wa mavazi yako mbele ya wafanyakazi wenzako ambao na wao wanajitahidi kuvaa mavazi ambayo yanawapendeza

Siku moja nilikuwa ofosini na baadhi ya wafanyakazi wenzetu wa kike walikuwa wakiwachambua wanaume ambao hawavai vizuri licha ya kuwa na uwezo wa kununua na kupangilia mavazi yao kulingana na miili yao

Wao walisema kwa jinsi wanavyoona wanaume waliopo pale ofisini kijana fulani (walimtaja jina ) kuwa ndiye kinara kwa kujipenda na kuvaa vizuri hapo ofisini na wengine walitamani kama angekuwa na uhusiano na wao kulingana tu anavyovaa na kupangilia mavazi yake


Mvazi pia humfanya bosi wako akupe safari za mara kwa mara ofisimi kwako na kukufanya hata wakati mwingine kupata kazi kutokana na mavazi ambayo unavaa kama kijana wa kisasa ambapo tumezoea kuona kuwa wanaume wengi hupenda mwanamke kutokana na mavazi ambayo mwanamke akivaa vizuri basi anavutia wanaume zaidi hali ambayo hata kwa wanawake nao huvutiwa na na jinsi wanaume wanavyovaa


Wapo wanawake ambao huamua kuwanunulia nguo waume zao pale wanapokwenda  makazini ili maradi tu na wao wanataka kuona kuwa waume ama wachumba zao wanakwenda na wakati kwa kuvaa mavazi ambayo kulingana na yeye mwanamke jinsi alivyo angependa mweza wake awe hivyo

Mfano wapo wanawake wanaopenda waume zao kuvaa suruali za jinsi,kadeti, ama za kitambaa lakini uchunguzi unaonesha zadi kuwa wanawake wengi hasa wa makamu na waliopata elimu hupendelea waume zao kuvaa suruali za kitambaa ili atapomtambulisha kwa wenzie aonekane anaenda na wakati

Kwa mwanaume yeyote yule lazima ajue kuwa mavazi ni muhimu katika kumfanya apate mweza bila ya wewe kutegemea  kwa kuwa wanawake huwa wanamuangalia kwa kina bila mwanaume kujua ambapo baadaye tu wengine huamua kujitokeza hadharani na kuwamabia mwanaume ukweli kuhusu jinsi anavyoajisikia juu yake

Msichana mmoja mkoani Dodoma aliwahi kumfuata kijana mmoja na kutaka awe na mahusiano naye ya mtu na mchumba wake ambapo msichana yule aliamua kumfuatilia mvulana yule kila siku alipokuwa akienda kanisani na ndio siku alipoamua kuandika barua rasmi na kumfuata mvulana yule hadi nyumbani kwao na kuwapa barua ndugu zake kuwa atapokuja apewe

Aliporudi alipewa barua hiyo ambayo iliandikwa kuwa kutokana na usafi na mavazi anayovaa ikiwemo na upangiliaji wa nguo zake yeye amevutiwa kuwa naye na hadi sasa mtaa mzima umejua kuwa yeye amemtongoza mwanaume na kwamba amekubali aibu hiyo iwe hadharani kwa ajili yake na haitaji fedha kutoka kwake

Watu walliokuwa mtaani hapo walistaajabu kusikia hilo lakini walikuwa hawana la kufanya kwani kila alipoulizwa juu ya hilo alikiri na kusema alishindwa kuvumilia kutokana na mavazi anayovaa mvulana huyo na alimua hivyo baada ya kila alipokuwa akimvizia hakupatikana na ndipo alipoomba ushauri kwa wenzake na kumshauri apeleke barua kwao ili mvulana yule ajue hilo kwani anaumia lakini hatoweza kumshawishi awe naye bila kufanya hivyo

No comments:

Post a Comment