KUVAA SHANGA... NI UREMBO AU? nipe jibu.
Watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu, nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..
skia story hii, "kuna
wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila
mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema
anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo
kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu.
kitu
cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba
wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake
akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo
juu..
ebu tuambieni wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi
wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani
ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na
ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni
mmakonde ndio inazidi kunichanganya..
sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....
No comments:
Post a Comment