Habari Mpya

Monday, 18 November 2013

Khadija Mwanamboka, balozi wa Oxfam aja na mradi mpya wa Kilimo


 MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA -KHADIJA MWANAMBOKA AMEZINDUA PROJECT-VVK-GROW CAMPAIGN PROJECT
 HII NI KAMPENI ILIYOBUNIWA NA KUENDESHWA NA BALOZI WA OXFAM KHADIJA MWANAMBOKA NA IKIWA NA LENGO LA KUAINISHA CHANGAMOTO ZA SOKO KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE.KUANIKA DHULUMA WANAYOFANYIWA WAKULIMA WA CHAKULA WANAWAKE NA KUHAMASISHA WATUMIAJI WA BIDHAA ZA CHAKULA MIJINI.KUTAMBUA THAMANI YA CHAKULA NA KUWA SOKO LENYE TIJA KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE
 KAMPENI HII INAHUSISHA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO -MODELS WATAKUWA WANAPITA KWENYE MIKUSANYIKO MBALI MBALI, MAOFISINI NA KWENYE TAASISI MBALI MBALI KUHAMASISHA NA KUUZA BIDHAA ZA WAKULIMA WADOGO WANAWAKE.
MWEZI WA NNE MWAKA HUU OXFARM ILIMTAMBULISHA MABALOZI WAKE WAPYA WA KAMPENI YA GROW. MBALI NA KHADIJA MWANAMBOKA WENGINE NI DINA MARIOS, MASOUD KIPANYA, SHAMIM MWASHA, HALIMA MDEE (MB), SHYROSE BHANJI (MB) NA JACOB STEPHEN 'JB'.
AMBAPO KILA BALOZI ATAKUJA NA MRADI WAKE UNAOHUSISHA CHAKULA NA KILIMO NA KHADIJA MWANAMBOKA AKIJA NA MRADI HUO ALIOUTAMBULISHA.
DM
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Khadija Mwanamboka, balozi wa Oxfam aja na mradi mpya wa Kilimo Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top