Habari Mpya

Wednesday 30 October 2013

Mavazi na mpangilio mzuri,unakufanya uonekane nadhifu,see this,



1. Jua unataka nini.
Hili ni jambo la kwanza la msingi ambalo mvaaji anatakiwa alifikirie  kwa ubakini kabla ya kufanya maamuzi ya baadaye. Zingatia muingiliano wa uhitaji wako na mahali husika wa vazi utakalo vaa. Kwa mfano, je vazi hilo wataka kulitumia kwenye sherehe, hafla au tafrija za namna gani?


2. jua umbo lako ili kufanya uchaguzi.
Kitu muhimu cha kuzingatia katika hili ni namna gani vazi ulilovaa linashabihiana na umbile la mwili wako. Kataa kabisa kuvaa nguo ambazo ni aidha zinakubana sajna au oversize ya mwili wako kwani hii yaweza kutoa taswira tata mbele ya wanajamii. 

3.Chagua Rangi.
Hapa waweza kuchagua rangi yoyote uipendayo kutokana na jinsi ya utashi wako unavyokutuma. Kama wewe ni mtu maarufu na unataka pengine watu wafahamu uwpo wako katika tukio Fulani basi crazy colours zinakufaa kama vile njano, nyekundu na blue .

4.Staili ya mavazi
Majarida, vipeperushi na mitandao ya tovuti ni sehemu nzuri za kufahamu mitindo mbali mbali ya mavazi. Amka na acha tabia ya kukariri mitindo ya mwaka 47, kumbuka vazi utakalovaa litakuwa ni ukumbusho wako  kwa vizaji vijavyo. 

5.Duka la Mavazi
Kumekuwa na ushindani mkubwa sana siku hizi katika ushindani wa maduka ya mavazi hususani nchini Tanzania nahii inakupa mwanya mkubwa kwa wewe mvaaji kuchagua bidhaa bora na kwa bei nafuu. Tambua kuwa vazi zuri si lazima liwe ni lile la gharama za juu peke yake bali hata yale mavazi utakayo nunua kwa wamachinga yanaweza kukutoa vizuri na ukapendeza 

6.Pambo za ziada (accesories).
Ili mvaaji aweze kungara zaidi atokapo na vazi lake mara njingi tunashauriwa kuwa na chaguzi sahihi za mapambo ya ziada yanayoendana na kile tulichokivaa kama vile heleni, mikufu,  mikoba, saa za mikononi, miwani, mitindo ya nywele na mengineyo yafananayo na hayo.




  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Mavazi na mpangilio mzuri,unakufanya uonekane nadhifu,see this, Description: Rating: 5 Reviewed By: fashion time na tatyana celestine
Scroll to Top