Habari Mpya

Thursday, 26 September 2013

Legging na uvaaji wake,yapaswa kuzingatia umri pia umbo .

Tasnia ya Mitindo inaendelea kukua siku hadi siku nao wanamitindo wanajitahidi kubuni aina tofauti za mitindo ili mradi tu kwenda na wakati,leo wametuletea mtindo mpya wa mavazi huitwao leggings.
hii ni maalum kwa wadada hasa wale wanaopenda kwenda na wakati lakini....................?

Vazi hili linataka mvaaji ajitambue kwa nini anavaa na ni wakati gani anatakiwakuvaa leggings, kwakua vazi hili linashika mwili basi inashauriwa kuangalia umri na saizi ya umbo lako ili uweze kuvaa na kujiskia comfortable.

Watu wenye umri kuanzia miaka 30 na kuendelea ili kulinda hesma yako basi unaweza kuvaa vazi hili na blauzi ndefu ili kufunika maeneo ya juu ya mvaaji.

pili epuka kuvaa legings mchana hasa kama umevaa na blauz fupi.na kama unajiona unanyama nyingi basi vaa vazi hili usiku ili kulinda hata utamaduni wa Mtanzania.

Mavazi haya yaliibuka sana miaka ya 90 na yalikua yakitumika zaidi kwa kufanyia mazoezi lakini sasa ndo viwalo, hata mjini tunavaa, hakikisha unazingatia jinsi ya uvaaji wa vazi hili ili kukulindia hesma yako.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Legging na uvaaji wake,yapaswa kuzingatia umri pia umbo . Description: Rating: 5 Reviewed By: Tatyana Celestine
Scroll to Top